Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC-USALAMA

Colombia: makubaliano kati ya waasi wa FARC na serikali

Waasi wa FARC na serikali ya Colombia wametangaza Jumatatu hii kuwa wamefikia makubaliano kuhusu suala la "kutendewa haki na kufidiwa kwa waathirika," ikiwa ni suala la nne kati ya sita katika ajenda ya mazungumzo yao ya amani yalioendeshwa kwa muda wa miaka mitatu.

Mkuu wa kundi la waasi wa FARC, Ivan Marquez (katikati) akiwasili katika mji wa Havana kwa mazungumzo ya amani na serikali, Desemba 12, 2015.
Mkuu wa kundi la waasi wa FARC, Ivan Marquez (katikati) akiwasili katika mji wa Havana kwa mazungumzo ya amani na serikali, Desemba 12, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Maudhui ya mkataba huu, ambayo yamekamilika baada ya karibu mwaka mmoja na nusu wa mazungumzo, yayawekwa wazi Jumanne wiki hii katika mji wa Havana, makao makuu ya mazungumzo kati ya raia wa Colombia yaliyofunguliwa mwezi Novemba 2012.

"Kesho tutahitimisha suala hili " waathirika " la ajenda ya mkataba mkuu", Marcos Calarca mmoja kati ya wajumbe wa waasi wa FARC katika mazungumzo hayo ametangaza mbele ya vyombo vya habari.

Kwa upande wake, ujumbe wa serikali, kwenye akaunti yake ya Twitter, umethibitisha kuhitimishwa kwa mkataba kuhusu suala hili muhimu la mazungumzo, ikikaribisha "hatua zaidi kwa kuelekea zoezi hili la kumaliza mgogoro."

Suala la "Waathirika" linalotazamia kutoa ukweli, kufidia, na dhamana kwa vitu ambavyo haviwezi kurekebishwa viliyoharibiwa katika machafuko, lilikua karibu kuhitimishwa, na pande husika katika mazungumzo hayo zimetangaza makubaliano kuhusu vyombo vya sheria baada ya uongozi wa mpito Septemba 23.

Lakini tofauti ziliibuka pia kati ya wajumbe kutoka pande hizo husika katika mazungumzo hayo kuhusu suala la "waathirika" ambalo linaamuru kuanzishwa kwa mahakama maalum na kuzuiliwa jela kwa wahusika wa makosa makubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.