Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC-Usalama

Colombia: FARC yakiri kumteka jenerali Alzate

Kufuatia tangazo la rais wa Colombia Juan manuel santos la kusitisha mazungumzo ya amani, baada ya kutekwa nyara afisa wa ngazi ya juu katika jeshi na watu wawili waliokua naye magharibi mwa Colombia, ujumbe wa waasi wa FARC umeendesha mkutano na vyombo vya habari.

Félix Antonio Muñoz (katikati), kiongozi wa kundi moja la waasi FARC, Magdalena Medio, akiwa pia mmoja kati ya wajumbe wa sekretarieti ya FARC akijieleza katika mkutano na vyombo vya habari, Novemba 18 mwaka 2014, Havane.
Félix Antonio Muñoz (katikati), kiongozi wa kundi moja la waasi FARC, Magdalena Medio, akiwa pia mmoja kati ya wajumbe wa sekretarieti ya FARC akijieleza katika mkutano na vyombo vya habari, Novemba 18 mwaka 2014, Havane. REUTERS/Enrique De La Osa
Matangazo ya kibiashara

FARC imethibitisha kuwashikilia watu watatu, akiwemo afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi la Colombia.

Mtu wa kwanza kutoa taarifa hiyo ya kushikiliwa kwa afisa huyo wa ngazi yajuu katika jeshi la colombia ni Félix Antonio Muñoz (kwa jina maarufu Pastor Alape), ambae ni kiongozi wa kundi moja la waasi hao, Magdalena Medio, akiwa pia mmoja kati ya wajumbe wa sekretarieti ya FARC.

Félix Antonio Muñoz, anatafutwa na Marekani kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya. Marekani ilitenga kitita cha Dola milioni mbili kwa atakayemkamata.

“ Ujumbe wa FARC katika mazungumzo ya amani umeelezea mshangao wake kufuatia tangazo la rais la kusitisha mazungumzo ya amani ya Havane", amesema Félix Antonio Muñoz.

Félix Antonio Muñoz, ameongeza kuwa: " Mchakato wa amani ambao maendeleo yake yameonesha matumaini ya maridhiano hayawezi kuingia hatarini kutokana na uamzi wa papo kwa hapo. Tunataka suala hili litatuliwa haraka iwezekanavyo ili mchakato uendelea kusonga mbele bila kikwazo hadi makubaliano ya mwisho".

Awali Félix Antonio Muñoz, alisema hawana taarifa yoyote kuhusu jenerali Alzate na watu wawili waliyokua naye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.