Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC-Usalama

Colombia: machafuko yaendelea kushuhudiwa Toribio

Wajumbe wawili wa jamii ya wazawa wa jimbo la Toribio wameuawa na waasi wa FARC katika mkoa kuo, kusini magharibi ya Colombia, ambapo mapigano kati ya waasi wa FARC na jeshi yamekua yakiibuka kila kukicha.

Wanajeshi wa Colombia wakipewa mafunzo ili waweze kulitokomeza kundi la waasi wa FARC, Florencia, Colombia.
Wanajeshi wa Colombia wakipewa mafunzo ili waweze kulitokomeza kundi la waasi wa FARC, Florencia, Colombia. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Jamii ya Wahindi wanaoishi eneo hilo wamesema wanatiwa wasiwasi na hali ambayo imekua tete.

Watu hao wameuawa wakati walipokua wakiondoa kwenye mabango picha ya kumbukumbu ya kiongozi wa waasi hao wa FARC, Alfonso Kano.

Jamii hiyo ya wahindi ishiyo katika mkoa huo wa Toribio inaendelea kuzingirwa na waasi wa FARC, huku ikiendelea kulindwa na watu asilia wa eneo hilo. Watu hao wazawa wa Toribio waliwahi kujadili na waasi wa FARC ili waweze kuondoa mabango hayo, bila mafaanikio.

Carlos Antonio Yatacué, ambaye ni mratibu wa ulinzi wa watu asilia wa mkoa wa Toribio, amebaini kwamba watu wanane miongoni mwa watuhumiwa wamekamatwa.

“ Baada ya tukio hilo kutokea, tuliomba msaada. Na tulilazimika kufukuzana nao hadi kwenye mlima mmoja ambapo tuliwakamata watuhumia wanane. Kwa mujibu wa mahakama yetu ya jadi watu hao wanakabiliwa na kifungo cha miaka 40”, amesema Carlos Antonio Yatacué.

Wakati huohuo serikali ya Colombia pamoja na rais Juan Manuel santos wamelani mauaji hayo. Rais Juan manuel Santo yuko ziarani barani Ulaya ili kuwashawishi viongozi wa Ulaya wamuunge mkono kwa mpango wake wa amani. Hata hivo Jamii ya Wahindi waishio Toribio wamesema hawaungi mkono mpango huo wa amani uliyoanzishwa na rais manuel Santo kwa sababu hawakushirikishwa. Jamii hiyo imeomba ishirikishwe katika mazungumzo ya amani yanayoendelea katika mji wa La Havane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.