Pata taarifa kuu
ARGENTINA-KUAPISHWA-SIASA

Argentina: Mauricio Macri aapishwa kuwa rais mpya

Mauricio Macri ameapishwa Alhamisi hii kama rais wa Argentina baada ya miaka 12 ya utawala wa wanandoa Kirchner, mabadiliko huenda yakashuhudiwa katika nyanja mbalimbali kwa sababu ameahidi kukuza uchumi na kukomesha vitendo vya kuzuia bidhaa kutoka nje.

Mauricio Macri akijianda kuapishwa kama rais wa Argentina, Desemba 10, 2015 katika mji wa Buenos Aires.
Mauricio Macri akijianda kuapishwa kama rais wa Argentina, Desemba 10, 2015 katika mji wa Buenos Aires. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Sherehe ilianza saa 5:30 saa za Argentina (sawa na 8:30 sasa za kimataifa), mbele ya wabunge na Maseneta. Rais huyo mpya kutoka chama cha mrengo wa kati kulia ameahidi kwamba serikali yake itatetea "bila kuchoka wale ambao wanaihitaji."

"Changamoto ni nyingi na hakuna kutatua matatizo usiku na mchana. Mabadiliko makubwa yanafanywa kwa kwenda hatua kwa hatua, hapana kila siku", rais mteule wa Argentina amesema.

Rais mpya ameelekea ikulu ya rais akishindikizwa na askari wake wa usalama. Katika Ikulu amekabidhiwa ukanda wa rais na amri ya uongozi wa taifa.

Marais na viongozi kadhaa wa serikali, hasa kutoka Amerika Kusini pamoja na Mfalme wa zamani wa Uhispania Juan Carlos, walikuwepo katika sherehe hiyo mjini Buenos Aires.

Kufuatia mgogoro na mrithi wake katika sehemu ya kukabidhiwa ukanda wa urais, rais wa zamani Cristina Kirchner hakuhudhuria sherehe hiyo, kutokana na amri ya mahakama ya kufupiza muhula wake ambao ungefikia mwisho katika masaa machache baadaye.

Miongoni mwa raia wa Argentina waliokusanyika mbele ya jengo la Bunge la Afrgentina, Susana Antonietti, mwenye umri wa miaka 60, alikuja akitokea Merlo, kitongoji cha Buenos Aires, kuhudhuria tukio hilo la kihistoria. "Tangu mwaka 1983 (mwisho wa udikteta) tuliona mambo mengi. Nina matumaini. Nataka rushwa ikomeshwe. Mimi siungi mkono chama cha Cristina Kirchner, rais anayemaliza muda wake”, amesema Antonietti.

Jamii ya wafanyabiashara imepongeza kuwasili madarakani kwa Meya wa mji wa Buenos Aires, ambaye alishinda urais kwa mshangao mkubwa. Macri alishinda katika duru ya pili ya uchaguzi kwa 51.33% ya kura dhidi ya 48.66% alizopata Daniel Scioli, mgombea wa muungano a vyama vya mrengo wa kushoto madarakani tangu mwaka 2003.

Macri, mwenye umri wa miaka 56, mhandisi na mwana wa bilionea kutoka Italia ambaye alipata bahati yake nchini Argentina, na aliweza kufuata nyayo za baba yake lakini baada ya miaka kumi katika uongozi wa kampuni Macri Group, aliingia katika siasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.