Pata taarifa kuu
MAREKANI-WAKIMBIZI-USALAMA

Marekani: Baraza la wawakilishi latishia kuwazuia wakimbizi wa Syria

Wabunge wa Marekani kutoka chama cha Republican wamemuomba Barack Obama kutowaruhusu wakimbizi kutoka Syria kuingia Marekani, na kutishia kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti wa kundi la Wabunge wa Marekani kutoka chama cha Republican, Paul Ryan, Novemba 3, Washington.
Mwenyekiti wa kundi la Wabunge wa Marekani kutoka chama cha Republican, Paul Ryan, Novemba 3, Washington. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao wamesema hayo, baada ya kupatikana kwa pasipoti ya raia wa Syria, karibu na mshambuliaji aliye jitoa mhanga katika Uwanja wa taifa wa michezo (Stade de France), baada ya mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu wengi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

"Kinga ni bora kuliko tiba", amesema mwenyekiti wa Wabunge kutoka chama cha Republican, Paul Ryan, baada ya siku tatu za mvutano wakisiasa nchini Marekani, ambaoo kulishuhudia zaidi ya nusu ya magavana na wagombea kutoka chama Republican katika Ikulu ya White House wakitangaza kukataa kuwapokea wakimbizi wa Syria, wakiwa na hofu ya kuzuka kwa mashambulizi kama yale yanayoshuhudiwa barani Ulaya.

Novemba 14, wakimbizi 2159 wa Syria walikubaliwa kuingia Marekani tangu 1 Oktoba 2011,kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani. Idadi ndogo ikilinganishwa na mamia ya maelfu ya watu wanaotafuta kuwasili barani Ulaya.

Lakini baada ya picha ya mtoto mdogo kutoka Syria, Aylan Kurdi, kufa maji katika bahari ya Mediterranean,na kuzua hali ya sintofahamu duniani kote, Barack Obama alisema mwezi Septemba kuwa anataka kuwapokea wakimbizi 10,000 wa Syria ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.