Pata taarifa kuu
MAREKANI-IS-USALAMA

Syria: mashambulizi ya anga ya Marekani yakimlenga"Jihadi John"

Jeshi la Marekani limeendesha mashambulizi ya anga Alhamisi wiki hii yakimlenga "Jihadi John", mpiganaji wa kundi la Islamic State (IS), ambaye anaonekana katika video akiwaua wafungwa, Pentagon imetangaza.

Moja ya habari iliogonga vichwa vya habari kwenye magazeti ya Uingereza Februari 27, 2015 ikimuonyesha "Jihadi John".
Moja ya habari iliogonga vichwa vya habari kwenye magazeti ya Uingereza Februari 27, 2015 ikimuonyesha "Jihadi John". AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Pentagon, Peter Cook, amesema hajajua kama Mohammed Emwazi, ambaye ni jina lake halisi, ameuawa. "Kwa sasa tufanya tathmini ya matokeo ya operesheni ya usiku huo (Alhamisi kuamkia Ijumaa) na tutatoa mtaarifa ya ziada katika njia sahihi", amesema katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa Pentagon, mashambulizi ya naga kutoka yameendeshwa katika mji wa Raqa, mji mkuu wa kundi hilo lenye msimamo mkali, kaskazini mwa Syria.

"Emwazi, raia wa Uingereza, alionekana katika video ilioonyesha mauaji ya waandishi wa habari wa Marekani Steven Sotloff na James Foley, mfanyakazi wa shirika la kihisani la Marekani, Abdul-Rahman Kassig, wafanyakazi wa mashirika ya kiutu ya Uingereza David Haines na Alan Henning, mwandishi wa habari wa Japan Kenji Goto na idadi kadhaa ya mateka wengine", taarifa ya uongozi wa jeshi la marekani imearifu.

Taarifa hiyo haielezi wazi iwapo mashambulizi hayo yameendeshwa na ndege za kawaida za kijeshi au ndege isio na rubani.

Mohammed Emwazi, anaye husika na programu za kompyuta kutoka London, alizaliwa Koweit kutoka familia ya watu wenye asili ya Iraq. Wazazi wake walihamia Uingereza mwaka 1993 baada ya kupoteza matumaini ya kupata uraia wa Koweit.

Kundi la Islamic State inadhibiti maeneo makubwa nchini Syria, ambayo inakabiliwa na machafuko tangu mwaka 2011, machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu 250,000, na nchini Iraq. Lakini mauaji hayo yanaonekana kupungua hivi karibuni kufuatia mashambulizi ya majeshi ya nchi hizo mbili na ndege za Urusi (nchini Syria) na muungano wa kimataifa ukiongozwa na Marekani (Syria na Iraq).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.