Pata taarifa kuu

Marekani: Rais wa China atazamiwa kufanya ziara ya kikazi Marekani Septemba 25

Rais wa Marekani Barack Obama anatazamia kumpokea mwenzake wa China Xi Jinping Septemba 25 katika Ikulu ya Marekani, huku kukiwa na wasiwasi juu ya kuporomoka kwa uchumi wa China lakini pia mvutano kuhusiana na madai ya uhalifu wa kimitandao.

Rais wa Marekani Barack Obama na mwenzake wa China Xi Jinping Novemba 12, 2014 Beijing.
Rais wa Marekani Barack Obama na mwenzake wa China Xi Jinping Novemba 12, 2014 Beijing. AFP/POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya kikazi ilikua imepangwa tangu miezi kadhaa iliyopita lakini tarehe yake sahihi, iliyotangazwa Jumanne wiki hii na serikali ya Marekani, ilikua bado haijatangazwa.

Ziara hii itaimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili lakini pia itakua fursa kwa viongozi wao kuanzisha mazungumzo kuhusu masuala ambayo hawakuweza kuafikiana katika hali ya maelewano kulingana na agenda iliochaguliwa kwa makini na Ikulu ya Marekani.

Mbali na vikao vya kazi, Barack Obama na mkewe Michelle watamkaribisha Rais wa China na mkewe, Peng Liyuan, kwa chakula cha jioni mbele ya wageni wengi..

Mkee wa Rais wa China, ni maarufu katika nchi yake tangu enzi zake za kuonekana katika vipindi mbalimbali vya televisheni viliyokua vikirushwa hewani katika kusheherekea Mwaka Mpya.

Ziara hii ya Rais wa China nchini Marekani inakuja wakati kuna ripotiwa mvutano kati ya China na Marekani, maafisa wa Marekani wanapendekeza uwezekano wa vikwazo dhidi ya raia wa China wanaotuhumiwa kufanya mashambulizi ya kimitandao katika ardhi ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.