Pata taarifa kuu
HAITI-MACHAFUKO-SIASA

UN yataka mazungumzo yapewe kipaumbele

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamehitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Haiti.

kwa muda wa siku tatu, ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umekutana kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo, wawakilishi wa upinzani na viongozi wa mashirika ya kiraia.
kwa muda wa siku tatu, ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umekutana kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo, wawakilishi wa upinzani na viongozi wa mashirika ya kiraia. REUTERS/Hannibal Hanschke/Files
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo wakati huu inashuhudiwa na machafuko, na kwa kipindi cha miaka minne sasa hakuna uchaguzi unaofanyika nchini humo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umekumbusha mchango wake katika mchakato wa kidemokrasia kupitia ujumbe wake unaosimamia amani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Porte-au-Prince, Amélie Baron, kwa muda wa siku tatu, ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umekutana kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo, wawakilishi wa upinzani na viongozi wa mashirika ya kiraia. Bunge limesitisha shughuli zake yapata majuma mawili kutokana na uchaguzi kutifanyika kwa wakati.

Mwakilishi wa Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Samantha Power, ameushinikiza kila upande kutautia suluhu tatizo hilo.

“ Tuko hapa kwa kuwaunga mkono raia wa Haiti, wala hatuko hapa kwa kuunga mkono upande fulani, lakini pia kuwa na mtazamo mzuri wa jinsi gani Umoja wa Mataifa unaweza kusaidia haiti”, amesema Samantha Power

Huu ni mwaka wa 10, ujumbe wa Umoja wa Mataifa ukiwa nchini Haiti. Viongozi wa haiti wameomba ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa kutopuguza idadi ya wafanyakazi wake kabla ya mchakato wa uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.