Pata taarifa kuu
Marekani-Afghanistan, Mexico

Wanajeshi wasiopungua 50 huuawa kila juma Afghanistan, Mexico kuteta na Marekani

Takriban Wanajeshi 50 mpaka 100 wa Afghanistan huuawa kila juma katika mapambano, hata hivyo hali hii imeelezwa kuwa haiashirii kuwa Vikosi vya nchi hiyo vimeshindwa,Luteni Jenerali wa Majeshi ya Marekani Mark Milley ameeleza.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Jumuia ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO vinafanya juhudi za kusaidia majeshi ya Afghanistan na Polisi nchini humo kuimarisha mbinu za kulinda usalama wa nchi hiyo.

Pamoja na matukio hayo ya mauaji vikosi vya Afghanistan vimeelezwa kuwa kulichukulia kama changamoto na kuwa hali hii haipotezi dhamira yao ya kupambana na Wanamgambo wa Taliban.

Jenerali Milley amesema kuwa ingawa Wanamgambo wa Taliban bado wanaonekana kuwa na nguvu, hawana uwezo wa kushinda vita hivyo na kuwawezesha kuidhibiti nchi hiyo baada ya kuondoka kwa majeshi ya NATO.

Wakati huohuo Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amesema kuwa atajaribu kufanya mazungumzo juma hili na Rais wa Marekani, Barack Obma juu ya Ripoti kuwa nchi hiyo imekuwa ikichunguza mawasiliano yake ya internet, na kuonya kuwa tukio hilo ni kinyume cha sheria.

Viongozi hao wawili watakutana ana kwa ana katika mkutano wa nchi 20 tajiri kiviwanda duniani ambao umeanza nchini Urusi hii leo.

Uamuzi huo wa Pena Nieto umekuja siku nne baada ya kuripotiwa kuwa Shirika la kijasusi la Marekani limekuwa likichunguza mawasiliano ya interneti kati ya Rais wa Brazil na Mexico.

Pena Nieto amesema kuwa hana shaka kuwa Wakati wa mkutano huo atapata walau nafasi ya kufanya mazungumzo na Rais Obama na kumweleza msimamo wake juu ya suala hilo, na kutoa wito kwa Marekani kufanya uchunguzi juu ya Ripoti hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.