Pata taarifa kuu
Canada-Afghanistani

Canada kuviondowa vikosi vyake nchini Afghanistani sambamba na vile vya Marekani na Ufaransa

Canada imemaliza miaka yake tisa ya Operesheni ya kijeshi nchini Afghanistan hii leo baada ya vifo vya wanajeshi mia moja na 57 hatua ambayo inaashiria kuondoka kwa majeshi ya Marekani na yale ya jumuia ya majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi,NATO.

Reuters/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kuondoka kwa takriban wanajeshi elfu 3 ambao wamekuwa na mapigano makali mji wa kandahar kumekuja wakati ambao vikosi vya magharibi vinatangaza kuondoka kabisa nchini Afghanistan ifikapo mwaka 2014.

mkuu wa majeshi ya Canada Brigedia generali Dean Milner amesema kwa miaka kadhaa majeshi na raia wa Canada wamekuwa wakijitoa katika operesheni hiyo,ingawa bado kuna kazi kubwa ya kufanya,wanajivunia kuwa operesheni yao imefanikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.