Pata taarifa kuu

COP15: Waandamanaji wadai 'hatua' kwa bioanuwai

Huko Montreal, maelfu ya watu wameandamana kwa wito wa baadhi ya mashirika sitini ya ulinzi wa mazingira pamoja na mashirika ya kiasili kutoka Canada na Marekani kutaka watoa maamuzi wanaokutana katika mkutano wa kimataifa wa COP15 kuchukua hatua "sasa kulinda bayoanuwai.

Maelfu ya watu waliandamana mjini Montreal huku wajumbe kutoka kote duniani wakiwa na hadi Desemba 19 kukubaliana kuhusu malengo muhimu ya kuhifadhi misitu, bahari na viumbe wa Dunia.
Maelfu ya watu waliandamana mjini Montreal huku wajumbe kutoka kote duniani wakiwa na hadi Desemba 19 kukubaliana kuhusu malengo muhimu ya kuhifadhi misitu, bahari na viumbe wa Dunia. REUTERS - CHRISTINNE MUSCHI
Matangazo ya kibiashara

Baridi kali ya mwezi wa Desemba inaonekana kuwakatisha tamaa kila mmoja, kwa sababu maandamano hayo ni ya ukubwa wa kawaida katika mitaa ya Montreal, anaripoti mwandishi wetu maalum huko Montreal, Pascale Guéricolas. 

Hata hivyo, lengo la uhamasishaji ni kutuma "ishara" kwa nchi ambazo zinajadili "mkataba unaofuata wa amani na asili". Wajumbe kote ulimwenguni wana hadi Desemba 19 kukubaliana juu ya malengo ishirini muhimu ya kukomesha uharibifu wa mazingira asilia ifikapo mwisho wa muongo huu.

Wakiwa mbele ya maandamano hayo, wawakilishi wa mataifa ya kiasili kutoka Chile, Canada Magharibi, lakini pia Ecuador, wanashutumu uchimbaji wa maliasili unaofanywa na makampuni makubwa ya uchimbaji madini.

Kwa sababu muda unasonga mbele, wanasema waandamanaji na mashirika yasiyo ya kiserikali: viumbe milioni moja vinatishiwa kutoweka, theluthi moja ya ardhi inaharibiwa vibaya na udongo wenye rutuba unatoweka, wakati uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya Tabia nchi yanaongeza kasi ya uharibifu wa bahari. "Ubinadamu umekuwa silaha ya kutoweka kwa watu wengi," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema katika mkesha wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa bayoanuwai, COP15.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.