Pata taarifa kuu

Mazungumzo ya Umoja wa Mataifa yameshindwa juu ya mkataba wa kulinda bahari kuu

Umoja wa Mataifa umeelzea masikitiko yake baada ya wanachama kushindwa kukamilisha mkataba unaopaswa kulinda bahari kuu. Kikao hiki cha tano cha mazungumzo kilimalizika bila kufikiwa makubaliano: washiriki hawakufaulu kushinda migogoro mingi mikubwa.

Eneo hili kubwa, ambalo linachukua karibu nusu ya sayari, linaanzia pale ambapo unaishia Ukanda Maalum wa Kiuchumi (EEZ) wa Mataifa na kwa hivyo hauko chini ya mamlaka ya nchi yoyote.
Eneo hili kubwa, ambalo linachukua karibu nusu ya sayari, linaanzia pale ambapo unaishia Ukanda Maalum wa Kiuchumi (EEZ) wa Mataifa na kwa hivyo hauko chini ya mamlaka ya nchi yoyote. ®Shutterstock
Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki cha tano kilikuwa cha mwisho, lakini licha ya mijadala iliyoendelea hadi Ijumaa jioni, haikutosha. Kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Umoja wa Mataifa umekuwa ukijaribu kuandaa, bila mafanikio, nakala ya kisheria yenye lengo la kulinda bahari kuu. Eneo hili kubwa, ambalo linachukua karibu nusu ya sayari, linaanzia pale ambapo unaishia Ukanda Maalum wa Kiuchumi (EEZ) wa Mataifa na kwa hivyo hauko chini ya mamlaka ya nchi yoyote.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekuwa zikifanya mazungumzo kwa miaka mingi ili kufikia makubaliano muhimu kwa ajili ya bahari, hazina hii dhaifu na muhimu kwa binadamu. Miongoni mwa masuala yenye utata ni mchakato wa kuunda maeneo ya hifadhi. Kutokuwepo kwa maafikiano katika hatua hii kunaweka mbali zaidi lengo kuu la kulinda angalau 30% ya sayari ifikapo 2030.

Hakuna makubaliano ama juu ya ugawaji wa faida inayowezekana kutokana na unyonyaji wa rasilimali za kijeni za bahari kuu ambapo viwanda vya dawa, kemikali na vipodozi vinatumai kugundua molekuli za miujiza au juu ya ugawaji wa faida zao zinazowezekana kwa nchi zinazoendelea ambazo, kwa kukosa maana yake, haiwezi kufanya utafiti wa gharama kubwa.

Shirika la kimataifa linalohusika na masuala ya mazingira, Greenpeace, limelaumu Umoja wa Ulaya, Marekani na Canada, ambao uchoyo wao wa kuweka rasilimali hizi ulichochea mazungumzo kuelekea kushindwa. Malipo yamekataliwa na mmoja wa wahawilishi wa Ulaya. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa sasa litaombwa kurejea kikao hiki cha tano katika tarehe ambayo bado haijaamuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.