Pata taarifa kuu
G20-CORONA-AFYA

Mawaziri wa afya wa G20 kupanga mkakati wa pamoja kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19

Mawaziri wa afya wa kundi la mataifa yaliyostawi kiuchumi ya G20, wanapanga kuwa na mkakati wa pamoja kukabiliana na janga la Covid-19, ambalo limeathiri nchi kadhaa, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 16,000 duniani.

Mawaziri wa afya wa kundi la mataifa yaliyostawi kiuchumi ya G20, yameanza mkutano tangu jumapili Aprili 19 kwa njia ya video kujadili mkakati wa pamoja wa kukabiliana na janga Covid-19.
Mawaziri wa afya wa kundi la mataifa yaliyostawi kiuchumi ya G20, yameanza mkutano tangu jumapili Aprili 19 kwa njia ya video kujadili mkakati wa pamoja wa kukabiliana na janga Covid-19. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri walikutana kupitia video Jumapili kujadili uwezekano huo kwa kudhibiti ugonjwa huo hatari, na watatoa taarifa ya pamoja baadae, G20 imesema katika taarifa.

G20 imesema kwamba mkutano na waandishi wa habari uliyopangwa hapo awali pia ulifutwa kutokana na kuwa Waziri wa Afya wa Saudi Arabia, nchi ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa G20, alitarajia hudhuria "mkutano wa dharura wa kundi linalopambana dhidi ya Covid-19 " katika nchi yake.

"Tunatambua kuwa kuna mada kadhaa za mjadala na tunafurahi kuzishughulikia katika makundi ya wafanyakazi wa afya ya baadaye," Waziri wa Afya wa Saudi Arabia, Tawfiq Al-Rabiah, amesema katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano, kulingana na video iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Amesema hatua za haraka ni pamoja na mahitaji ya ushirikiano na kujitolea kwa mashirika ya kimataifa kuhusu mkakati uliyoratibiwa kwa janga la Covid-19, kwa msisitizo wa kusaidia nchi zinaohitaji na kuwekeza katika utafiti na ugunduzi wa kutengeneza teknolojia, vifaa, chanjo na dawa.

Waziri huyo wa Saudi Arabia pia amebaini juu ya kuundwa kwa kundi la wafanyakazi ulimwenguni kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, kitovu cha uvumbuzi wa kubadilishana maarifa na kundi la viongozi katika suala la usalama wa wagonjwa ili kutoa mkakati wa pamoja kwa kupunguza hatari kwa usalama wa mgonjwa.

Viongozi wa Uhispania, Singapore, Jordani na Uswizi walialikwa kuhudhuria mkutano huo Jumapili, na pia mashirika ya kimataifa na kikanda, pamoja na Shirika la Afya Duniani na Benki ya Dunia, kulingana na taarifa ya awali ya G20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.