Pata taarifa kuu
MGOMO-HAKI

Chad: Walimu watangaza kuzindua tena mgomo wao miezi miwili baada ya masomo kuanza tena

Chama cha Walimu nchini Chad (SET) kimerejelea mgomo wake leo Ijumaa Machi 15, baada ya Mkutano Mkuu uliofanyika siku moja kabla. Harakati za kushutumu ahadi za mamlaka zisizotekelezwa zilisitishwa mwezi Januari, baada ya miezi miwili na mashauriano na Waziri Mkuu Succès Masra. Lakini makubaliano hayakufuatwa, kulingana na SET.

Shule ya Kiarabu ya Sultan Kasser, huko Ndjamena.
Shule ya Kiarabu ya Sultan Kasser, huko Ndjamena. RFI/Raphaëlle Constant
Matangazo ya kibiashara

Ili kuashiria kuanzishwa tena kwa mgoo huo miezi miwili baadaye, SET imeamua kurudisha magunia matano ya nafaka kwa serikali. Haya yalitolewa na Waziri Mkuu ili kuhakikisha imani nzuri ya serikali katika mikataba iliyofanywa na chama hicho cha waalimu.

Lakini makubaliano ya mishahara, marupurupu na kazi hayakufuatiwa na kutekelezwa, kulingana na mwenyekiti wa kamati ya kutatua mgogoro ya SET, Faustin Djimoudouel.

Walituwekea ahadi kuhusiana na hoja zetu saba za madai, na tukagundua kwamba, katika suala la mazungumzo, wakati mwenzako anajikubalisha jambo, itabidi pia umsikilize. Kwa nia yetu njema ilibidi tuisikiliza serikali yetu ambayo ilijitolea. Lakini, tangu kuanza kwa masomo Januari 8, 2024 hadi leo, tumeona kwa masikitiko kwamba hakuna kinachofanyika ili kupunguza mawazo ya walimu. Mamlaka haitaki kabisa kufanya mazungumzo ya uwazi nasi. Na tulielewa mchezo mara moja, watu wanavutiwa zaidi na maswali ya kisiasa na sio maswali ya kielimu. Tumependelea kuweka chaki chini na kubaki nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.