Pata taarifa kuu

Libya: Uamuzi wa kutoza ushuru wa sarafu ya Libya dhidi ya dola wapingwa vikali

Nchini Libya, mzozo wa fedha unaendelea. Aguila Saleh, rais wa Baraza la Wawakilishi lililoko Tobruk, mashariki mwa Libya, aliamua siku ya Alhamisi Machi 14, 2024 kupunguza thamani ya dinari ya Libya, kwa kutoza ushuru wa 27% kwa ununuzi wa fedha za kigeni. Kwa hivyo, kodi mpya inadhoofisha kiwango cha ubadilishaji kutoka dinari 4.80 za Libya kwa dola moja hadi kati ya dinari 5.95 na 6.15 kwa dola moja.

Benki kuu ya Benghazi, Septemba 23, 2020.
Benki kuu ya Benghazi, Septemba 23, 2020. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Tatizo la msingi la Libya ni kuongezeka kwa usawa wa kifedha. Nchi ina karibu chanzo kimoja tu cha mapato, ambacho ni mafuta. Bei ya pipa imedorora katika miezi ya hivi karibuni, na matarajio yanayotarajiwa zaidi hayajumuishi dhana ya kuiona ikifikia kizingiti cha dola 90. Hatua iliyopunguzwa kwa wakati na ambayo haifai kuendelea, kulingana na Aguila Saleh, zaidi ya mwaka wa 2024. Hata hivyo, uamuzi huo umepingwa vikali na wabunge ambao wametishia kuchukua hatua za kisheria.

Hatua hii ya kurekebisha kiwango cha ubadilishaji wa dinari dhidi ya fedha za kigeni ilifuata pendekezo lililopingwa kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu, Al-Seddik Al-Kabir. Ombi lake limethibitishwa na haja ya "kukidhi mahitaji ya soko kwa fedha za kigeni" na kupunguza "ugumu unaopatikana na Benki Kuu". Uamuzi huo unaweza, amesema, kutoa mapato ya karibu dola bilioni 12, ambayo inaweza kupunguza baadhi ya athari za deni la umma.

Lakini uamuzi huo umeibua hasira miongonimwa wabune na kuupina vikalie. Fawzi al Nouwairi, Makamu wa Kwanza wa Spika wa Baraza la Wawakilishi, anapinga hilo. Anatoa wito wa kuondolewa mara moja kwa hatua hii "ya uwongo" ambayo "matokeo" yake yatakuwa "janga".

Takriban wabunge wengine thelathini wametia saini ombi la kutaka kuangaliwa upya kwa uamuzi huo, ambao "si wa haki" na kinyume cha sheria kwa sababu haupigiwi kura na wabune na ambao, zaidi ya hayo, unahimiza matumizi ya nje ya bajeti ya serikali.

Wanauchumi kutoka Chuo Kikuu cha Benghazi, ambao Spika wa Bunge aliomba ushauri, walitoa maoni yasiyofaa ambayo ni wazi hayakuzingatiwa.

Hata hivyo, Libya iliishinda Nigeria Februari mwaka jana katika suala la uzalishaji wa mafuta na kuwa nchi inayoongoza kwa uzalishaji barani Afrika. Kuhusu matumizi ya fedha za umma, ilifikia rekodi ya dinari bilioni 165 mwaka 2023. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Libya imeshutumu ukosefu wa uwazi wa matumizi yake

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.