Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Chad: Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais kufanyika Mei 6

Upigaji kura kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Chad utafanyika Mei 6, Tume Taifa ya Uchaguzi (ANGE) imetangaza siku ya Jumanne wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Uchaguzi huu utaashiria mwisho wa kipindi cha mpito na mamlaka ya Mahamat Idriss Déby Itno, aliyeteuliwa kuwa mkuu wa utawala wa kijeshi unaoongozwa na majenerali 15 baada ya kifo cha baba yake Idriss Déby Itno.
Uchaguzi huu utaashiria mwisho wa kipindi cha mpito na mamlaka ya Mahamat Idriss Déby Itno, aliyeteuliwa kuwa mkuu wa utawala wa kijeshi unaoongozwa na majenerali 15 baada ya kifo cha baba yake Idriss Déby Itno. © AURELIE BAZZARA-KIBANGULA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa urais nchini Chad utafanyika Mei 6, Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (ANGE) imetangaza siku ya Jumanne, uchaguzi ambao utamaliza kipindi cha mpito kilichodumu kwa miaka mitatu. Mahamat Idriss Déby Itno alitangazwa kuwa rais wa kipindi cha mpito, akiwa mkuu wa utawala wa kijeshi unaoongozwa na majenerali 15, baada ya kifo cha baba yake Idriss Déby Itno, aliyejeruhiwa vibaya na waasi katika uwanja wa vita mnamo mwaka wa 2021.

Mara moja aliahidi kurudisha mamlaka kwa raia kwa kuandaa uchaguzi miezi 18 baadaye, tarehe ambayo hatimaye iliahirishwa kwa miaka miwili. Mwisho wa kipindi cha mpito nchini Chad uliahirishwa hadi Oktoba 10, 2024. "Mbali na tarehe hii (Oktoba 10), nchi itaanguka katika ombwe la kisheria, sawa na machafuko yanayotabirika. Kwa hivyo ni muhimu kudumisha uchaguzi kabla," ametangaza mwenyekiti wa ANGE Ahmet Bartchiret.

"ANGE imeanzisha ratiba halisi na inayoweza kufikiwa ambayo imeundwa hasa katika mambo yafuatayo: Mei 6, 2024, kufanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais," ametangaza Bw. Bartchiret. Rais Déby, hata hivyo, alitangaza mbele ya Umoja wa Afrika kkwamba hatagwania katika uchaguzi wa urais ujao, lakini katikati ya mwezi wa Desemba Katiba mpya iliyopitishwa na kura ya maoni hatimaye ilimruhusu kugombea.

"Ukoo wa Deby kusalia madarakani"

Upinzani, ambao ulitoa wito wa kususia uchaguzi huo, ulipinga vikali matokeo hayo, ukitaja "kunyang'anywa mamlaka". Pia ulikosoa uteuzi wa mkuu wa ANGE, wa Mahakama ya Katiba na Mahakama ya Juu, vyombo vinavyohusika na migogoro ya uchaguzi na uthibitishaji wa matokeo.

Mahamat Déby pia anaweza kutegemea Patriotic Salvation Movement, chama cha wengi kilichoanzishwa na hayati babake, ambaye alimteua kama mgombea wake kwa uchaguzi wa urais. Vyama vya upinzani vinahofia "ukoo wa Deby" kuendelea kushikili mamlaka ya nchi katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati, nchi ya pili kwa maendeleo duni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kabla ya mtoto wake, Idriss Déby Itno aliongoza nchi hii kutoka mwaka 1990 hadi kifo chake mnamo mwaka 2021.

Maandamano ya upinzani yamepigwa marufuku kimfumo tangu yale yaliyokandamizwa kwa umwagaji damu mnamo Oktoba 22, 2022. Kati ya watu 100 na 300 walipigwa risasi na kuuawa na polisi. Kufuatia maandamano haya, viongozi wengi wa upinzani walilazimika kwenda uhamishoni, akiwemo Succès Masra, Waziri Mkuu wa sasa na rais wa Transfoma, chama cha zamani cha upinzani cha kisiasa. Bwana Masra alirejea mwaka mmoja tu baadaye, kutokana na makubaliano ya maridhiano ambayo yalimaliza mvutano na upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.