Pata taarifa kuu

Chad yatangaza hali ya dharura ya chakula huku kukiwa na wimbi la wakimbizi wa Sudan

Chad imetangaza "hali ya dharura ya chakula na lishe" knchini kote, kwa mujibu wa agizo lililotangazwa kwa umma siku ya Ijumaa katika mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, ambapo zaidi ya wakimbizi nusu milioni wamemiminika katika kipindi cha miezi kumi wakikimbia vita nchini Sudan.

Chad, ambayo inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan, tayari ilihifadhi zaidi ya 400,000 kabla ya mzozo mpya.
Chad, ambayo inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan, tayari ilihifadhi zaidi ya 400,000 kabla ya mzozo mpya. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Agizo la rais wa mpito, Mahamat Idriss Déby Itno, lililotiwa saini siku ya Alhamisi, halina maelezo zaidi juu ya hatua zilizotekelezwa wala idadi ya watu wanaohusika, lakini Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) lilionya mwezi wa Novemba mwaka jana kuhusu "kusitishwa" kwa misaada yake kutokana na wimbi la wakimbizi wa Sudan ikiwa litashindwa kukusanya fedha zinazohitajika za kimataifa.

WFP kisha ilitoa "msaada wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.4" nchini Chad, idadi ya wakimbizi wa ndani na wakimbizi katika nchi hii iliyo nusu jangwa huko Afrika ya Kati, kutokana na migogoro inayoendelea katika eneo lake na majirani zake, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Niger, Nigeria, Libya na Cameroon.

Lakini tangu kuanza, Aprili 15, 2023, vita nchini Sudan kati ya jeshi la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wakiongozwa na mpinzani wake, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, wakimbizi wapya 546,770 wamewasili Chad, kulingana na takwimu za hivi punde mwanzoni mwa mwezi wa Februari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Chad, ambayo inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan, hasa kutoka Darfur wanaokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 2003 katika eneo hili la mashariki mwa Sudan, tayari ilimwahifadhi zaidi ya 400,000 kabla ya mzozo mpya. Kwa jumla, nchi hii, iliyoainishwa na Umoja wa Mataifa kama ya pili kwa maendeleo duni, inapaswa idhibiti zaidi ya "watu 1,570,000 waliolazimika kuyahama makazi yao", wakiwemo zaidi ya wakimbizi milioni 1.1. Wengine ni wakimbizi wa ndani, kutokana na uasi wa makundi mbalimbali yenye silaha dhidi ya utawala wa kijeshi wa Jenerali Déby.

"Mnamo mwezi wa Desemba, WFP italazimika kusitisha msaada wake kwa watu waliokimbia makazi na wakimbizi kutoka Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Cameroon, kutokana na ukosefu wa fedha. Kuanzia mwezii wa Januari 2024, usitishaji huu utaongezwa (... ) wakimbizi wapya kutoka Sudan, ambao hawatapokea chakula", shirika la Umoja wa Mataifa lilibainisha tarehe 21 Novemba. "Ili kuhakikisha uungwaji mkono unaoendelea kwa watu walioathiriwa na mgogoro nchini Chad katika kipindi cha miezi sita ijayo", linaangazia "hitaji la dharura la dola milioni 185".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.