Pata taarifa kuu

Mmoja vinara wa mashirika ya kiraia atekwa nyara

Mmoja wa viongozi wa mashirika ya kiraia nchini Burkina Faso, Bassirou Badjo, alitekwa nyara siku ya Jumatano huko Ouagadougou na "watu waliojitambulisha kama maafisa" wa serikali, shirika lake limetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Tangu mwaka wa 2015, Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na ghasia za wanajihadi zinazohusishwa na vuguvugu la watu wenye silaha wenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State.
Tangu mwaka wa 2015, Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na ghasia za wanajihadi zinazohusishwa na vuguvugu la watu wenye silaha wenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State. U.S. Africa Command - Sgt. Benjamin Northcutt
Matangazo ya kibiashara

 

"Februari 21 alasiri", Bassirou Badjo, "afisa katika Kurugenzi Kuu ya Mshikamano wa Kitaifa na Usaidizi wa Kibinadamu (DGSAH) yenye makao yake makuu mjini Ouagadougou, alitekwa nyara (mahali pake pa kazi)," limetangaza vuguvugu la Balais Citoyen ambalo Bw. Badjo ni mwanachama.

Wahusika wa utekaji nyara huo ni "watu waliojitambulisha kama mmaafisa wa usalama wa serikali" na kumpeleka "mahali pasipojulikana", imesema vuguvugu la Balai Citoyen, ambalo "linataka" "kuachiliwa" kwake.

Siku ya Jumanne, mwanaharakati mwingine wa Balai Citoyen, Rasmane Zinaba, pia alitekwa nyara "kutoka nyumbani kwake" na "watu wasiojulikana wakiwa walivalia kiraia na wakiwa na silaha", kabla ya kupelekwa "mahali pasipojulikana", liliandika vuguvugu hilo siku kisa hicho kilipotokea, pia likitaka "aachiliwe bila kuchelewa".

Bassirou Badjo na Rasmane Zinaba ambo ni nguzo ya Balai Citoyen, vuguvugu la kiraia ambalo lilisababisha kuanguka kwa utawala wa Rais wa zamani Blaise Compaoré mwaka wa 2014,  wote walitakiwa na utawala wa kijeshi wa Burkina Faso kushirikiana na jeshi katika vita dhidi ya ghasia za kijihadi zinazoikumba nchi hiyo. Bw. Zinaba aliwasilisha malalamiko yake katika mahakama ili iweze kufuta ombi hili.

Kesi kadhaa za utekaji nyara kwa viongozi wanochukuliwa kuwa mahasimu wa serikali ya kijeshi iliyo madarakani tangu mapinduzi ya mwezi Septemba 2022, yaliyoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré, zimeripotiwa katika miezi ya hivi karibuni huko Ouagadougou. Mnamo Februari 15, mawakili nchini Burkina Faso walisitisha kazi, kutaka kuachiliwa kwa mmoja wao, Guy Hervé Kam, aliyetekwa nyara mwishoni mwa mwezi wa Januari na kuzuiliwa na mamlaka ya Burkina Faso.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, wapinzani kadhaa "walitakiwa" "kushiriki" katika mapambano dhidi ya wanajihadi. Baadhi, kama vile aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Ablassé Ouedraogo, au mwanaharakati wa haki za binadamu Daouda Diallo, walionekana mwezi Februari katika video isiyo na tarehe wakiwa na silaha, wakiwa wamevalia sare ya jeshi, katika eneo la msituni.

Tangu mwaka wa 2015, Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na ghasia za wanajihadi zinazohusishwa na vuguvugu la watu wenye silaha lenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State, ambalo limesababisha vifo vya takriban watu 20,000 na zaidi ya milioni mbili wakiwa wakimbizi wa ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.