Pata taarifa kuu

Wanasheria wagoma wakitaka 'kuachiliwa' kwa mwenzao anayezuiliwa nchini Burkina Faso

Wanasheria nchini Burkina Faso wamefanya mgomo siku ya Alhamisi, na kuzorotesha shughuli za mahakama nyingi, wataka kuachiliwa kwa mwenzao aliyetekwa nyara mwishoni mwa mwezi Januari na wanaume waliovalia kiraia na kuzuiliwa na mamlaka ya Burkina Faso, amebainisha mwandishi wa habari kutoka shirika la habari la AFP.

Luteni Kanali Yacouba Isaac Zida (kushoto) Guy Hervé Kam (kulia), wakili wa vuguvugu la "allet citoyena", akizungumza katika kambi ya kijeshi huko Ouagadougou Oktoba 31, 2014. Naibu Kamanda kikosi cha walinzi wa rais wa Burkina Faso Luteni Kanali Isaac Zida alisema Jumamosi alichukua mamlaka baada ya rais aliyepinduliwa Blaise Compaoré kuripotiwa kuukimbia mji mkuu.
Luteni Kanali Yacouba Isaac Zida (kushoto) Guy Hervé Kam (kulia), wakili wa vuguvugu la "allet citoyena", akizungumza katika kambi ya kijeshi huko Ouagadougou Oktoba 31, 2014. Naibu Kamanda kikosi cha walinzi wa rais wa Burkina Faso Luteni Kanali Isaac Zida alisema Jumamosi alichukua mamlaka baada ya rais aliyepinduliwa Blaise Compaoré kuripotiwa kuukimbia mji mkuu. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

 

"Chama cha Wanasheria, katika kikao chake kisicho cha kawaida cha Februari 7, 2024, kiliamua kusimamisha kazi Alhamisi Februari 15 nchini kote Burkina Faso, kama sehemu ya hatua zilizochukuliwa kutaka kuachiliwa huru bila masharti ya mwenzao, Guy Hervé Kam", aliandika kiongozi wa chama cha Wanasheria nchini Burkina Faso, Siaka Niamba, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Kwa hivyo wanasheria wanaalikwa kuacha kushiriki katika kesi mbele ya mahakama zote bila ubaguzi," alisisitiza.

Wakijibu wito wake, mawakili wa Burkina Faso wamesusia kazi katika mahakama mbalimali na nyumba ya wakili huko Ouagadougou siku ya Alhamisi. Vyumba ambako kunasikilizwa kesi mbalimbali katika mahakama ya mji mkuu wa BurkinaFaso vilibaki tupu, shirika la habari la AFP limebaini.

Wakili Guy Hervé Kam, aliyetekwa nyara usiku wa Januari 24 kuamkia 25 kwenye uwanja wa ndege wa Ouagadougou na wanaume waliovalia kiraia, tangu wakati huo anazuiliwa katika majengo ya idara ya usalama wa taifa, kwa "kupuuza kwa makusudi na bila kujali masharti yanayohakikisha uhuru wa wakili", kulingana na Chama cha Wanasheria nchini Burkina Faso.

Anajulikana sana nchini Burkina Faso kwa kuwa wakili wa familia ya Thomas Sankara, mkuu wa zamani wa nchi (1983-1987) aliyeuawa wakati wa mapinduzi yaliyofanywa na mrithi wake Blaise Compaoré.

Hakimu wa zamani, wakili Kam pia ni kiongozi wa shirika la kiraia nchini Burina Faso. Ni mmoja wa walioanzisha vuguvugu la "Balai Citoyen", vuguvugu ambalo lilichukua jukumu muhimu katika kuanguka kwa serikali ya Blaise Compaoré mnamo mwaka 2014.

Kesi kadhaa za utekaji kwa watu wanachukuliwa kama mahasimu dhidi ya serikali ya kijeshi iliyo madarakani tangu mapinduzi ya Septemba 2022, yaliyoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré, zimeripotiwa katika miezi ya hivi karibuni huko Ouagadougou.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ablassé Ouédraogo alitekwa nyara mwishoni mwa mwezi wa Desemba na mkuu wa zamani wa jeshi, Luteni Kanali Évrard Somda, mwezi Januari.

Serikali ya mpito ilidai mnamo Januari kuwa ilizuia jaribio jingine la kuvuruga utulivu na kuanzisha msako dhidi ya mtandao unaohusisha wanajeshi na raia.

Tangu mwaka wa 2015, Burkina Faso inakabiliwa na ghasia za wanajihadi zinazohusishwa na vuguvugu la watu wenye silaha lenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State, ambalo limesababisha vifo vya takriban watu 20,000 na zaidi ya milioni mbili wakimbizi wa ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.