Pata taarifa kuu

Burkina Faso yasitisha uuzaji nje wa dhahabu zinazochimbwa kienyeji

Burkina Faso imesitisha mauzo yake ya dhahabu na vitu vya thamani kutoka kwa uzalishaji wa kienyeji, ili "kupanga vyema" sekta hiyo, Waziri wa Nishati na Madini ametangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumatano.

Mwezi Novemba, rais wa mpito aliye madarakani tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso, Ibrahim Traoré, alitangaza kuwa "dhahabu imekuwa bidhaa namba moja ya nje" ya nchi hiyo.
Mwezi Novemba, rais wa mpito aliye madarakani tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso, Ibrahim Traoré, alitangaza kuwa "dhahabu imekuwa bidhaa namba moja ya nje" ya nchi hiyo. © Capture d'écran/le MondeAfrique.fr/ AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Burkina Faso imeamua "kusimamisha uidhinishaji wa usafirishaji wa dhahabu na vitu vingine vya thamani vya uzalishaji wa kienyeji", uamuzi ambao ulianza kutekelezwa siku ya Jumanne, ameandika Waziri Yacouba Zabré Gouba.

Kusimamishwa huku kunatokana na hitaji la usafi wa mazingira katika sekta ya (madini) na kunaonyesha nia ya serikali ya kupanga vyema uuzaji wa dhahabu na vitu vingine vya thamani," ameongeza. Katika kipindi hiki cha kusimamishwa, ikiwa ni pamoja na muda haukutajwa," wahusika wa madini ambao wana kiasi cha kuuza nje wanatakiwa kuwasiliana na Chama cha Kitaifa cha Vitu vya Thamani (Sonasp) ambao watawajibika kuzilipa", ameongeza.

Mwezi Novemba, rais wa mpito aliye madarakani tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso, Ibrahim Traoré, alitangaza kuwa "dhahabu imekuwa bidhaa namba moja ya nje" ya nchi hiyo. Burkina Faso ina migodi 17 ya dhahabu ya viwandani, mitano kati yake imefungwa kwa sababu zinazohusishwa na ghasia za mara kwa mara za wanajihadi ambazo zinadhoofisha nchi.

Uzalishaji wa dhahabu katika nchi hii, ambao unachangia karibu 14% kwa mapato ya taifa la Burkina Fasoe, ulipungua kwa 13.7% mnamo mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka 2021, kutoka tani 66.8 hadi 57.6, kulingana na takwimu rasmi. Sekta ya ufundi inazalisha uzalishaji wa ziada wa kila mwaka wa takriban tani 10 za dhahabu, kulingana na Wizara ya Madini.

Mwishoni mwa mwezi wa Novemba, mamlaka ya mpito iliyotokana na mapinduzi nchini Burkina Faso ilizindua ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kusafisha dhahabu, chenye uwezo wa kuzalisha tani 150 za dhahabu safi kwa mwaka kwa 99.99%, au karibu kilo 400 za dhahabu kwa siku. Mnamo mwezi wa Februari 2023, serikali ya Burkina Faso pia iliomba kilo 200 za dhahabu zinazozalishwa na kampuni tanzu ya kampuni ya acanada ya Endeavor Mining kwa "mahitaji ya umma".

Burkina Faso imekuwa ikipigana tangu mwaka 2015 dhidi ya makundi ya kijihadi yenye mafungamano na Islamic State na Al-Qaeda ambayo pia yameshambulia nchi jirani za Mali na Niger, nchi mbili zinazotawaliwa pia na tawala za kijeshi na ambazo Ouagadougou imejiunga nazo katika miezi ya hivi karibuni

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.