Pata taarifa kuu

Niger, Burkina, Mali: sarafu ya pamoja inayowezekana kuepuka 'ukoloni', asema Tiani

Mkuu wa utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi ya kijeshi nchini Niger alizungumza Jumapili jioni kuhusu uwezekano wa kuunda sarafu ya pamoja na Burkina Faso na Mali, kama "hatua" ya kuondokana na "ukoloni".

Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Niger Abdourahamane Tiani kwenye televisheni ya taifa, Agosti 19, 2023.
Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Niger Abdourahamane Tiani kwenye televisheni ya taifa, Agosti 19, 2023. Β© ORTN
Matangazo ya kibiashara

Β 

"Fedha ni hatua ya kuondokana na ukoloni huu," alisema mkuu wa utawala wa kijeshi wa Niger Abdourahamane Tiani kwenye televisheni ya taifa ya Niger, akimaanisha faranga ya CFA na Ufaransa, nchi iliyotawala Niger katika enzi za ukoloni.

Niger, Mali na Burkina Faso - nchi tatu zilizotawaliwa katika enzi za ukoloni na Ufaransa, ambazo kwa sasa zinaendeshwa na serikali za kijeshi -, zilizowekwa ndani ya Muungano wa Nchi za Sahel (AES), "zina wataalam (wa fedha) na kwa wakati ufaao, tutaamua," aliongeza.

"Fedha ni ishara ya uhuru," alibainisha Jenerali Tiani, na Mataifa ya AES "yanashiriki katika mchakato wa kurejesha uhuru wao kamili." Anahakikisha kwamba "hakuna tena suala la Mataifa yetu kuwa ng'ombe wa maziwa wa Ufaransa".

Kiongozi wa Niger hakutoa maelezo juu ya uwezekano wa mzunguko wa sarafu ya siku zijazo. Hii inaweza, ndani ya AES, kuchukua nafasi ya faranga ya CFA, ambayo kwa sasa ni ya pamoja kwa nchi nane wanachama wa Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (UEMOA), ikiwa ni pamoja na Niger, Burkina Faso na Mali.

Ukosoaji mkali ulioandaliwa na nchi hizi tatu za Saheli na wafuasi wao dhidi ya faranga ya CFA pia unaweza kuwafanya kuondoka UEMOA.

Mnamo mwezi wa Novemba, Mawaziri wa Uchumi na Fedha wa AES walipendekeza hasa kuundwa kwa hazina ya kuleta utulivu na benki ya uwekezaji.

Kauli ya Jenerali Tiani inakuja wiki mbili baada ya Mali, Burkina Faso na Niger kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS, nchi 15), ambazo wanazituhumu kwa kutumiwa na Ufaransa.

ECOWAS ilipinga mapinduzi ya kijeshi katika nchi hizo tatu na hasa kuweka vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Mali, kabla ya kuvitekeleza dhidi ya Niger.

Mwezi Agosti, ilifikia hatua ya kutishia kuingilia kijeshi nchini Niger kurejesha utulivu wa kikatiba na kumwachilia rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum, ambaye bado yuko kizuizini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.