Pata taarifa kuu

ECOWAS yataka umoja baada ya kudhoofika kutokana na migogoro

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), iliyokumbwa na migogoro mingi, imezindua wito wa umoja baada ya mkutano wa dharura kuhusu hali nchini Senegal na tangazo la kujiondoa kwa nchi tatu wanachama zinazoongozwa na tawala za kijeshi zilizotokana na mapinduzi.

Moja ya mamlaka ambayo ECOWAS inayo ni kuweka vikwazo vizito vya kiuchumi, kama ilivyofanya dhidi ya Mali na Niger kufuatia mapinduzi ya hivi karibuni.
Moja ya mamlaka ambayo ECOWAS inayo ni kuweka vikwazo vizito vya kiuchumi, kama ilivyofanya dhidi ya Mali na Niger kufuatia mapinduzi ya hivi karibuni. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Majadiliano ya faragha yamefanyika kwa saa kadhaa siku ya Alhamisi kabla ya washiriki kumaliza kikao hiki kisicho cha kawaida kilichowaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi kutoka nchi wanachama. Taarifa ya mwisho kwa vyombo vya habari bado inatarajiwa Ijumaa.

Omar Alieu Touray, rais wa Tume ya ECOWAS, ameelezea mzozo wa Senegal, ulioanzishwa kutokana na kuahirishwa kwa ghafla kwa uchaguzi wa rais kutoka Februari 25 hadi Desemba 15, kama "maendeleo ya wasiwasi" kabla ya kuzindua wito wa umoja kati ya nchi wanachama. "Kama kuna wakati ambapo ECOWAS lazima ibaki na umoja, ni sasa," amesema mwanadiplomasia huyu wa Gambia katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Mkuu wa Baraza la Usuluhishi na Usalama la shirika la kikanda Yusuf Maitama Tuggar, kwa upande wake, alizitaka Niger, Mali na Burkina Faso kubadili mwelekeo na kutoondoka katika Jumuiya ya Afrika Magharibi. Alionya kwamba kujiondoa kwa nchi tatu za Saheli kutasababisha matatizo zaidi "kwa raia wa kawaida". ECOWAS inawahakikishia raia wa nchi 15 wanachama uwezo wa kusafiri bila visa na kujiimarisha katika nchi wanachama kufanya kazi au kuishi huko.

Tangazo la wiki jana la kujiondoa kwa Burkina Faso, Niger na Mali limezua wasiwasi miongoni mwa mamia kwa maelfu ya raia wa nchi hizi, watu binafsi na wafanyabiashara. "Tuna nguvu pamoja, kama jumuiya," alisisitiza Bw. Tuggar, pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria.

Lakini haikuwa wazi siku ya Ijumaa iwapo ECOWAS imechukua hatua zozote - na ikiwa ni hivyo, ni zipi - kuhusiana na migogoro mbalimbali ambayo inaweka uaminifu wake hatarini. Rasimu ya ajenda ya mkutano wa Alhamisi ilikuwa imejumuisha mzozo wa Senegal pamoja na tangazo la kujiondoa kwa nchi tatau wanamemba wa ECOWAS.

Baada ya mkutano huo, rais wa Tume ya ECOWAS ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Baraza hilo halijajadili uhalali wa kikatiba wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wa Senegal. "Lazima tubaini uhalali wa katiba au ukiukaji wa katiba (wa kuahirishwa huku) kabla ya kuchukua au kuweka vikwazo," aliongeza. "Hili lazima lifanyike na hatujajadili," amebainisha.

"Bahati mbaya"

Moja ya mamlaka ambayo ECOWAS inayo ni kuweka vikwazo vizito vya kiuchumi, kama ilivyofanya dhidi ya Mali na Niger kufuatia mapinduzi ya hivi karibuni. Wataalamu wanaamini, hata hivyo, kwamba Senegal bado iko mbali na hatua hii.

Mawaziri kutoka Senegal walihudhuria mkutano wa Alhamisi, tofauti na wenzao kutoka Burkina, Mali, Niger na Guinea, waliosimamishwa kutoka ECOWAS baada ya mapinduzi.

Tangazo la kujiondoa kwa nchi tatu za Saheli ni "bahati mbaya", Rais wa Benin Patrice Talon alisema siku ya Alhamisi. "Ilinisikitisha sana. Nilizungumza na mmoja wa wakuu watatu wa nchi husika na nikamwambia kuwa haikuwa sawa." "Uamuzi huu unawaadhibu watu" na "hakuna migogoro kati ya watu wa ECOWAS", amesisitiza.

Siku ya Jumanne ECOWAS iliitaka Senegal, maarufu kama mmoja wa wanafunzi wazuri wa muungano huo, "haraka" kurejesha kalenda ya urais. Umoja wa Ulaya, ukiafikiana na Jumuiya ya Afrika Magharibi, ulitoa wito wa kurejeshwa hadi Februari 25. Mshirika mwingine, Marekani, anaonaa kura ya kuahirisha uchaguzi kuwa kinyume cha sheria.

Washirika hawa wa Senegal walionyesha wasiwasi wao juu ya hatari ya machafuko, lakini pia kwa pigo kwa mazoezi ya kidemokrasia ambayo Senegal inatajwa kwa urahisi kama mfano katika ukanda ambapo fitina na utimilifu hufuatana.

"Tunasikia ujumbe huu," Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Ismaïla Madior Fall alisema siku ya Jumatano jioni kutoka Nigeria kwenye televisheni ya Ufaransa France 24, "lakini leo tunapendelea mantiki ya kisiasa ya ndani."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.