Pata taarifa kuu

Burkina Faso, Mali na Niger wanasema wanataka kuondoka ECOWAS sasa

Siku kumi baada ya kutangaza kuondoka katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Burkina Faso, Mali na Niger zimebaini siku ya Jumatano kwamba wanakusudia kuondoka sasa na sio mwaka mmoja kama ilivyoainishwa na azimio la ECOWAS.

Mkutano usio wa kawaida wa ECOWAS mjini Accra, Ghana, tarehe 17 Agosti 2023.
Mkutano usio wa kawaida wa ECOWAS mjini Accra, Ghana, tarehe 17 Agosti 2023. AFP - GERARD NARTEY
Matangazo ya kibiashara

 

Nchi hizo tatu zilitangaza kujiondoa mnamo Januari 28 na kutuma arifa rasmi kwa jumuiya hii siku iliyofuata. Ibara ya 91 ya mkataba wa ECOWAS inaeleza kuwa nchi wanachama zitaendelea kuwa chini ya wajibu wao kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kuarifu kujiondoa. Tarehe ya mwisho ambayo nchi tatu zinazoongozwa na tawala za kijeshi ambazo ziliingia mamlakani kupitia mapinduzi hazikusudii kutii.

"Serikali ya Jamhuri ya Mali haihusishwi tena (na) masharti ya tarehe ya mwisho yaliyotajwa katika Ibara ya 91 ya mkataba," inasisitiza Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali katika barua kwa ECOWAS, ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi iku ya Jumatano. Bamako inadai kuwa ECOWAS yenyewe ilifanya mkataba huo kuwa "usiofanya kazi" iliposhindwa kutimiza wajibu wake kwa kufunga mipaka ya nchi wanachama na Mali mnamo mwezi wa Januari 2022, na kuinyima ufikiaji wa bahari.

ECOWAS wakati huo ilikuwa imeweka vikwazo vizito kwa Mali ili kulazimisha wanajeshi walio madarakani kujitolea kwa ratiba inayokubalika ya kukabidhi madaraka kwa raia. Wizara "inasisitiza hali isiyoweza kutenduliwa ya uamuzi wa serikali" wa kujiondoa "bila kuchelewa kutoka kwa ECOWAS kutokana na jumuiya hiyo kukiuka nakala zake."

Nchini Burkina Faso, barua kama hiyo kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje iliyotumwa kwa ECOWAS inasisitiza "uamuzi wa kujiondoa bila kuchelewa" na "hali yake isiyoweza kutenduliwa". Ouagadougou inataja "mapungufu makubwa" ya ECOWAS na hasa "vikwazo" vilivyochukuliwa kwa "nia ya wazi ya kuharibu uchumi wa nchi katika kipindi cha mpito".

Hatimaye huko Niamey, mamlaka ya Niger pia imethibitisha kujitoa kwao mara moja kutoka kwa ECOWAS katika barua iliyotumwa kwa jumiya hiyo wiki iliyopita, na kuzingatia Ibara ya 91 kuwa imepitwa na wakati, kulingana na chanzo cha serikali kilichohojiwa na shirika la habari la AFP. ECOWAS inatazamiwa kufanya mkutano wa ngazi ya mawaziri mjini Abuja siku ya Alhamisi kujadili hali ya kisiasa na usalama katika eneo hilo.

 

Mali, Niger na Burkina Faso, ambako serikali za kiraia zimepinduliwa na mapinduzi ya kijeshi mfululizo tangu mwaka 2020, zimesimamishwa kutoka kwa mamlaka ya ECOWAS, ambayo ilijaribu bila mafanikio kuwalazimisha raia kurejea madarakani.

ECOWAS ilifikia hatua ya kutishia matumizi ya nguvu nchini Niger, ambapo jeshi lilimpindua rais mteule Mohamed Bazoum. Lakini mataifa hayo matatu yalikuja pamoja na kuunda Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES), yaliyowekwa chini ya ishara ya uhuru na umoja wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.