Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Nigeria: Tisa wauawa katika ghasia zingine katika Jimbo la Plateau

Takriban watu tisa wameuawa katika mashambulizi matatu katika eneo la Bokkos katikati mwa Nigeria, wiki kadhaa baada ya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya takriban watu 200 katika eneo hilo, serikali ya eneo hilo imesema siku ya Alhamisi.

Jimbo la Plateau, ambalo linapatikana kati ya kaskazini mwa Nigeria yenye Waislamu wengi na kusini yenye Wakristo wengi, mara kwa mara hukumbwa na milipuko ya ghasia za kikabila na kidini.
Jimbo la Plateau, ambalo linapatikana kati ya kaskazini mwa Nigeria yenye Waislamu wengi na kusini yenye Wakristo wengi, mara kwa mara hukumbwa na milipuko ya ghasia za kikabila na kidini. © Photo Audu MARTE / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Siku ya Jumatano, watu watano waliuawa walipokuwa wakifanya kazi katika mashamba yao huko Butura Kampani. Siku hiyo hiyo, watu wengine watatu pia waliuawa kwenye shamba lao la viazi nyuma ya chuo kikuu," Monday Kassah, mwenyekiti wa baraza la la serikali la Bokkos, eneo Jimbo la Plateau ameliambia shirika la habari la AFP.

Milio ya risasi ilisikika katika mashamba nyuma ya Chuo Kikuu cha Jimbo la Plateau eneo la Bokkos siku ya Jumatano alasiri, kulingana na Azi Peter, mfanyakazi katika taasisi hiyo. Siku ya Jumanne, mwanamume kutoka jamii ya Fulani pia aliuawa katika kijiji kimoja cha Butura Kampani, Kassah ameongeza.

Hakuna ushahidi wa kutambua wazi washambuliaji wa mashambulizi haya, kulingana na mamlaka ya ndani. Jimbo la Plateau, ambalo linapatikana kati ya kaskazini mwa Nigeria yenye Waislamu wengi na kusini yenye Wakristo wengi, mara kwa mara hukumbwa na milipuko ya ghasia za kikabila na kidini.

Eneo hili hivi karibuni limekuwa likilengwa na mashambulizi makubwa ambayo yalisababisha hasira nchini lakini pia ndani ya jumuiya ya kimataifa. Wakati wa Krismasi, watu wenye silaha walishambulia karibu vijiji ishirini katika wilaya za Bokkos na Barkin Ladi, na kuua watu wasiopungua 198, kulingana na mamlaka katika Jimbo la Plateau.

Ingawa jimbo hilo mara kwa mara huwa eneo la mivutano na vurugu kati ya wakulima na wafugaji wa kuhamahama, mamlaka haijashutumu kundi lolote kuhusika na mashambulizi haya. "Tuna wasiwasi kuwa kila siku raia wetu wanashambuliwa na kuuawa. Kila mara tunaripoti kesi zetu kwa idara za usalama. Mauaji pekee hayataleta amani ya kudumu katika jamii," Umar Ori, mkuu wa chama cha wafugaji huko Bokkos (MACBAN) ameliambia shirika la habari la AFP.

Nchini Nigeria, wakazi wa mikoa ya kaskazini-magharibi na kati pia wanaishi katika hofu ya mashambulizi ya makundi ya kijihadi na magenge ya wahalifu ambao hupora vijiji na kuua au kuteka nyara wakaazi wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.