Pata taarifa kuu

Wawili wafariki na wengine karibu 80 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea nchini Nigeria

Takriban watu wawili waliuawa na 77 kujeruhiwa Jumanne jioni katika mlipuko mbaya uliotokea katika mji wa Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, mamlaka ya eneo hilo imetangaza siku ya Jumatano, ikitaja mlipuko wa bahati mbaya.

Mlipuko huo, ambao ulitokea muda mfupi kabla ya saa mbili usiku katika wilaya ya Bodija na kuharibu karibu majengo 25 kulingana na Nema, ulizua hali ya hofu miongoni mwa wakazi.
Mlipuko huo, ambao ulitokea muda mfupi kabla ya saa mbili usiku katika wilaya ya Bodija na kuharibu karibu majengo 25 kulingana na Nema, ulizua hali ya hofu miongoni mwa wakazi. Daily Trust/Jeremiah Oke
Matangazo ya kibiashara

 

"Kufikia sasa tumerekodi majeruhi 77, wengi wao wametibiwa, na vifo viwili," amesema Seyi Makinde, gavana wa Jimbo la Oyo ambalo Ibadan ndio mji mkuu wa jimbo hilo, katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandaowa X (zamani ukiitwaTwitter).

Idadi hiyo inaweza kuongezeka wakati shughuli za uokoaji zikiendelea Jumatano asubuhi, kulingana na Saheed Akiode, mratibu wa ukanda wa kusini-magharibi katika Idara ya Huduma za Dharura (Nema).

Mlipuko huo, ambao ulitokea muda mfupi kabla ya saa mbili usiku katika wilaya ya Bodija na kuharibu karibu majengo 25 kulingana na Nema, ulizua hali ya hofu miongoni mwa wakazi.

Kulingana na gavana huyo, shahidi za kwanza za uchunguzi " zilitaja kwamba wachimbaji haramu waliokuwa wakimiliki moja ya nyumba za Bodija walikuwa wamehifadhi vilipuzi vilivyosababisha mlipuko huo."

Kwenye eneo la tukio, mwandishi wa habari wa AFP aliweza kuona uharibifu mkubwa: eneo hilo lilikuwa limefunikwa na vifusi, majengo kadhaa karibu na eneo la tukio yaliharibiwa sana na magari yaliharibiwa kabisa, moja gari lilitupwa juu ya lingine.

Gavana huyo amesema serikali itatoa makazi ya muda na kuhakikisha walioathirika wanapokea "msaada wa kujenga upya maisha yao."

Ibadan ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Nigeria ikiwa na zaidi ya wakazi milioni 3.5, baada ya Lagos na Kano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.