Pata taarifa kuu

Chad: Upinzani wamtaka Déby kujiuzulu na washushia lawama Ufaransa

Upinzani usio na silaha nchini Chad siku ya Jumatano umemtaka rais wa mpito Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, ambaye alichukua mamlaka kufuatia kifo cha babake mwaka 2021, kuacha kugombea katika uchaguzi ujao wa urais, uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2024.

Waandamanaji wa vuguvugu la Wakit Tamma wakishikilia bendera ya Ufaransa wakati wa maandamano.
Waandamanaji wa vuguvugu la Wakit Tamma wakishikilia bendera ya Ufaransa wakati wa maandamano. © DJIMET WICHE/AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Jukwaa kuu la upinzani na mashirika ya kiraia, Wakit Tamma, wanashutumu "jumuiya ya kimataifa", hususan Ufaransa, kwa kuunga mkono "mrithi wa kifalme" katika uongozi wa nchi hii ya Sahel na kumuongezea nguvu Mahamat Déby katika " nia yake ya kumiliki utawala, ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu.

Akiwa na umri wa miaka 37, Mahamat Déby alitangazwa na jeshi mnamo Aprili 20, 2021 kuwa rais wa mpito akiwa mkuu wa utawala wa kijeshi unaoongozwa na majenerali 15, baada ya kifo cha baba yake Idriss Déby Itno aliyeuawa na waasi alipokuwa akielekea kwenye uwanja wa vita. Alitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 30 baada ya kuchukua mamlaka kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Kunyakua madaraka kwa jenerali huyo kijana kulilaaniwa kwa nguvu na jumuiya ya kimataifa ambayo, hususan Ufaransa, Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU), zilimtaka arejeshe mamlaka kwa raia mwishoni mwa kipindi cha mpito cha miezi 18. kama alivyojikubalisha hadharani kufuatia kifo cha baba yake. Miezi kumi na minane baadaye, utawala wa kijeshi ulirefusha kipindi cha mpito kwa miaka miwili kwa pendekezo la mazungumzo ya kitaifa yaliyosusiwa na upinzani wa kisiasa na wenye nguvu zaidi kati ya vuguvugu nyingi za waasi wenye silaha.

Mwishoni mwa wa Desemba, Katiba mpya ilipitishwa kufuatia kura ya maoni iliyoafikiwa na asilimia 86 ya ndiyo, lakini ikasusiwa na upinzani. Sheria mpya ya kimsingi inamruhusu Mahamat Déby kugombea katika uchaguzi ujao wa urais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka. Na chama kikuu kilichoanzishwa na babake, Patriotic Salvation Movement (MPS), kilimteua Jumamosi kuwa mgombea wake.

Jenerali Déby "kutokana na wajibu wa kizalendo", anapaswa kukataa kupitishwa na chama chake cha MPS kuwania kiti cha urais, Wakit Tamma imeandka katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP siku ya Jumatano. Wakit Tamma imelaani "nia" ya Mahamat Déby "kumrithi baba yake". "Kwa baraka za jumuiya ya kimataifa" ambayo iliweka mbele "maslahi ya ubinafsi" imesema, ikitoa mfano wa EU na AU.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.