Pata taarifa kuu

Katiba mpya ya Chad yapitishwa moja kwa moja

Mahakama ya Juu ya Chad imeidhinisha siku ya Alhamisi matokeo ya kura ya maoni ya katiba mpya iliyoandaliwa na utawala wa kijeshi ulio madarakani kwa muda wa miaka miwili na nusu, hatua muhimu inayotarajiwa kuandaa njia ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2024 nchini humo.

Upinzani, ambao ulitoa mwito mkubwa wa kususia, ulishutumu "mapinduzi ya pili ya Mahamat Idriss Déby Itno" na matokeo ambayo si ya kuaminika.
Upinzani, ambao ulitoa mwito mkubwa wa kususia, ulishutumu "mapinduzi ya pili ya Mahamat Idriss Déby Itno" na matokeo ambayo si ya kuaminika. © AFP - DENIS SASSOU GUEIPEUR
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo ya mwisho,  "Ndiyo" ilishinda kwa 85.90% ya kura wakati "Hapana" ilipata 14.10% ya kura na kiwango cha ushiriki ambacho kilifikia 62.8%, amebainisha jaji kiongozi wa Mahakama ya Juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Kwa sehemu ya upinzani na mashirika ya kiraia, matokeo ya uchaguzi huu ni sawa na kura ya maoni iliyokusudiwa kutayarisha uchaguzi wa rais wa mpito, Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno. Mahakama ya Juu ilitupilia mbali rufaa ya Kambi ya Shirikisho, muungano wa upinzani ambao ulikuwa umeomba kubatilishwa kwa matokeo kutokana na kasoro kadhaa za kufanyika kwa uchaguzi.

Upinzani, ambao ulikuwa umetoa wito mkubwa wa kususia, umeshutumu, kulingana na Max Kemkoye, rais wa Kundi la Ushauri la Watendaji wa Kisiasa (GCAP), "mapinduzi ya pili ya Mahamat Idriss Déby Itno", mbele ya matokeo ambayo, kulingana na yeye, si ya kuaminika. Nakala ya katiba mpya hayatofautiani sana na yale ambayo tayari yanatumika na bado yanatoa madaraka makubwa kwa mkuu wa nchi.

Akiwa na umri wa miaka 37, Mahamat Déby alitangazwa na jeshi mnamo Aprili 20, 2021 kuwa rais wa mpito akiwa mkuu wa utawala wa majenerali 15, baada ya kifo cha baba yake Idriss Déby Itno aliyeuawa na waasi alipokuwa akielekea vitani. Alitawala nchi kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 30.

Jenerali huyo kijana aliahidi uchaguzi baada ya kipindi cha mpito cha miezi 18 na akatoa ahadi kwa Umoja wa Afrika kwamba hatoshiriki. Miezi kumi na minane baadaye, serikali yake iliongeza kipindi cha mpito kwa miaka miwili na kumruhusu kuwa mgombea katika uchaguzi wa rais uliopangwa mwishoni mwa mwaka 2024.

Katika maadhimisho ya miezi 18 ya mpito, Oktoba 20, 2022, kati ya vijana mia moja na zaidi kwa jumla ya 300 waliuawa kwa kupigwa risasi huko N'Djamena na polisi na wanajeshi, kulingana na upinzani na mashirika yasiyo ya kiserikali ya nchini Chad na ya kimataifa. Walikuwa wakiandamana kupinga nyongeza ya miaka miwili. Zaidi ya elfu moja walifungwa kabla ya kusamehewa, lakini kadhaa waliteswa au kutoweka, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali na upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.