Pata taarifa kuu

Baraza la Katiba lamkatisha tamaa Sonko kuwania katika uchaguzi ujao

Baraza la Katiba la Senegal siku ya Ijumaa limekataa katu katu kiongozi wa upinzani anayezuiliwa jela Ousmane Sonko kugombea katika uchaguzi wa urais,kwa madai kuwa faili lake halijakamilika kutokana na kuondolewa kwake kwenye orodha ya wapiga kura kufuatia kukutwa na hatia mwezi Juni katika kesi ya maadili.

Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Mei 2023.
Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Mei 2023. © Capture AFPTV
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Katiba la Senegal limefutilia mbali kugombea kwa mwanasiasa wa upinzani Ousmane Sonko katika uchaguzi wa urais wa Februari 25 kwa misingi kwamba faili lake halijakamilika, wakili wake Me Ciré Clédor Ly amewambia waandishi wa habari. "Tulipoingia, Mwenyekiti (wa Baraza) Badio Camara ametufahamisha mara moja kwamba faili (ya Bw. Sonko) haikuwa kamilifu," amesema, bila kutaja stakabadhi zinazokosekana.

Utawala ulikataa kumpa kiongozi huyo wa upinzani nyaraka zote muhimu kwa ajili ya kugombea kwake, kwa hoja kwamba aliondolewa kwenye orodha za uchaguzi baada ya kuhukumiwa mwezi Juni katika kesi ya maadili. Lakini timu yake hata hivyo iliwasilisha barua ya kuwania katika uchaguzi kwa Baraza la Katiba. Siku ya Alhamisi jioni, Mahakama ya Juu ilithibitisha kifungo cha miezi sita jela dhidi ya Ousmane Sonko kwa kukashifu wazitri wa utalii, hukumu inayoonekana kumfanya asiwezi kuwaia katika uchaguzi wa urais.

Katika utaratibu mwingine, Bw. Sonko alipatikana na hatia mnamo Juni 1 ya uasherati wa mtoto mdogo na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani. Mpinzani hakufika kwenye kesi hiyo na alipatikana na hatia bila kuwepo. Amekuwa gerezani tangu mwisho wa mwezi wa Julai kwa mashtaka mengine, ikiwa ni pamoja na kuitisha uasi, na analaani mashitka haya yote kama njama zinazolenga kumuondoa kwenye uchaguzi wa urais.

Kambi ya Sonko ilipata matumaini ya kiongozi wao kuwania kwenye kiti cha urais baada ya jaji kuagiza asajiliwe tena kwenye orodha za wapiga kura katikati ya mwezi wa Desemba. Masuala ya kisheria ya kiongozi huyu wa upinzani, anayependwa sana na vijana, yametatiza maisha ya kisiasa ya Senegal tangu mwaka wa 2021 na kusababisha matukio kadhaa ya machafuko mabaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.