Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-HAKI

Senegal: Ousmane Sonko awasilisha faili yake ya kugombea kwa Baraza la Katiba

Ousmane Sonko amewasilisha faili yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais kwa Baraza la Katiba. Mwanasiasa huyo wa upinzani nchini Senegal, ambaye anazuiliwa jela tangu mwisho wa mwezi Julai mwaka huu, aliamua kupuuzia utawala wa Senegal, ikiwa ni pamoja na Kurugenzi Kuu ya Uchaguzi, ambayo inamkatalia kutoa fomu za udhamini, miongoni mwa wengine. Hii saa chache kabla ya kumalizika kwa mawasilisho ya wagombea kwenye Baraza la Katiba.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko huko Dakar mnamo Machi 2021.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko huko Dakar mnamo Machi 2021. AP - Sylvain Cherkaoui
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Dakar, Birahim Touré

“Tumewasilisha faili yetu kwenye Baraza la Katiba! »: haya ni maneno ya Ayib Daffé, mwakilishi wa mpinzani Ousmane Sonko, ambaye hata hivyo anakataa kusema ikiwa ni yeye mwenyewe aliyetekeleza kitendo hiki, kilichofanywa siri tangu Jumapili iliyopita.

Kwa hakika, hata wanahabari wanaosimama kizembe mbele ya makao makuu ya Baraza la Katiba wanadai kutomuona mwakilishi rasmi wa Ousmane Sonko wala kupokea maoni yoyote kutoka kwake, kama ilivyo kawaida kwa wadhamini wanapotoka katika ofisi ya karani wa mahakama.

Kulingana na chanzo kutoka kwa chama kilichofutwa, PASTEF, ni maagizo yalitolewa kwa lengo hili.

Njia ya "kugeuza usikivu wa utawala mkuu ambao hata ulikataa kukubali amana na fomu za udhamini za mgombea wetu", kulingana na mpatanishi wetu.

Kuondolewa kwa Ousmane Sonko kwenye orodha za uchaguzi na Wizara ya Mambo ya Ndani kulifutwa hivi majuzi na mahakama kuu ya Dakar. Mawakili wa serikali wametangaza kukata rufaa kupinga hukumu hii. Hali ambayo inaweza kumuweka nje ya kinyang'anyiro cha urais mnamo Februari 25, 2024.

Wagombea wote katika uchaguzi huu walikuwa hadi saa sita usiku Jumatatu kuamkia Jumanne kuwasilisha stakabadhi zao za kugombea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.