Pata taarifa kuu
SHERIA-SIASA

Senegal: Hatia yathibitishwa kwa Ousmane Sonko, ambaye hatoshiriki kwa uchaguzi ujao wa urais

Mahakama ya Juu ilithibitisha mnamo Alhamisi Januari 4 hukumu iliyotolewa Mei mwaka jana na Mahakama ya Rufaa ya kifungo cha miezi sita jela kwa Ousmane Sonko kwa kumkashifu Waziri wa Utalii Mame Mbaye Niang. Mpinzani huyo hataweza kugombea katika uchaguzi wa rais mwezi ujao, hata kama wanasheria wake wakiendelea kuwa na matumaini ya kukata rufaa.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, hapa ilikuwa Dakar mnamo Machi 8, 2021.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, hapa ilikuwa Dakar mnamo Machi 8, 2021. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Uamuzi wa Mahakama ya Juu umetolewa Alhamisi usiku, muda mfupi kabla ya saa sita usiku, baada ya takriban saa 12 za kusikilizwa ambapo mawakili wa pande zote mbili walibishana kwa muda mrefu kwa ajili ya wateja wao, ambao hawakuwepo.

Mawakili wa Ousmane Sonko - 13 kwa jumla - kwanza waliomba isipokuwa ukiukaji wa katiba, ikimaanishwa waliomba Mahakama ya Juu iondoe kesi hiyo kwa kupendelea Baraza la kikatiba.

Kisha waliomba kubatilishwa kwa hukumu ya Mahakama ya Rufaa ya Mei 8, wakitaja dosari nyingi za kiutaratibu. Kama wito wa kuripoti mahaamani ambao mteja wao hakupokea.

Hoja zilizochukuliwa kwa sehemu na mwanasheria mkuu ambaye alikuwa akiunga mkono kufutiliwa mbali kwa hukumu hiyo, lakini zikakataliwa na jaji ambaye kwa hivyo alidumisha hukumu ya Ousmane Sonko ya kifungo cha miezi 6 na fidia ya faranga milioni 200 za CFA. Na ambaye pia alifutilia mbali uvunjaji wa katiba.

Suala la siku hii bila shaka lilikuwa ni kustahiki kwa mpinzani. Mmoja wa wanasheria wake alizungumza kuhusu "uamuzi wenye utata". Kulingana na mawakili wake na kanuni za uchaguzi, hukumu hii ya mwisho inamfanya Ousmane Sonko kutostahiki kwa miaka mitano. Kwa hivyo hataweza kushiriki katika uchaguzi wa urais wa Februari 25.

Upande wa mashitaka wakataa tamaa

Ousmane Sonko alihukumiwa baada ya kukata rufaa kifungo cha miezi sita jela kwa kumkashifu na kumtusi hadharani Mame Mbaye Niang. Meya wa Ziguinchor alikuwa amemshutumu Waziri wa sasa wa Utalii hadharani kwa kutajwa katika ripoti ya Ukaguzi Mkuu wa Jimbo kwa madai ya ubadhirifu. Kiongozi wa Wazalendo wa Kiafrika wa Senegal kwa kazi, maadili na udugu (PASTEF), mwenye umri wa miaka 49, ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019, alihukumiwa mnamo mwezi Machi 2023 katika mahakama ya mwanzo kifungo cha miezi miwili jela, na kutakiwa kulipa faranga za CFA milioni 200 (karibu. 300,000 euro)kama fidia. Katika utaratibu mwingine, Ousmane Sonko alipatikana na hatia mnamo Juni 1 ya "ufisadi wa vijana" na alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Mwishoni mwa kusikilizwa kwa kesi hiyo, mawakili wa Ousmane Sonko walikatishwa tamaa, hasa kwa kuwa kabla ya hukumu wa mahakama, walikuwa na matumaini waliposikiliza matakwa ya mwanasheria mkuu. "Nimekata tamaa sana. Kila mtu alifuata matakwa ya mwendesha mashtaka wa umma, na matakwa haya yalilenga kufutwa kwa jumla ya hukumu yote kwa uvunjaji mkubwa wa sheria,” amesema Wakili Ciré Clédor Ly.

Kuhusu wakili wa Mame Mbaye Niang, tunasema "tumeridhishwa sana" kwamba uamuzi wa Mahakama ya Rufaa bado haujabadilika. “Uliona kuwa maswali mengi ya kisheria yaliulizwa. Majaji walijibu maswali yote yaliyoulizwa. Hatimaye, kila kitu kilithibitishwa, ina maana kwamba wakati mtu hajalipa, huwekwa gerezani. Kila kitu kimethibitishwa, kwa hivyo tuna furaha,” amesema Me El Hadji Diou, wakili Mame Mbaye Niang.

Baraza la Katiba litachapisha orodha ya mwisho ya wagombeawa uchaguzi mnamo Januari 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.