Pata taarifa kuu

Mahakama ya Juu ya Senegal yatoa uamuzi kuhusu kesi ya Ousmane Sonko kwa kumkashifu waziri

Mahakama ya Juu ya Senegal imetoa uamuzi siku ya Alhamisi kuhusu kifungo cha miezi sita jela kilichositishwa kwa kosa la kumkashifu Ousmane Sonko na uamuzi wake unaweza kuhatarisha uwezekano wa mpinzani aliyefungwa kutoshiriki katika uchaguzi wa rais wa Februari 25.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko huko Dakar mnamo Machi 2021.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko huko Dakar mnamo Machi 2021. AP - Sylvain Cherkaoui
Matangazo ya kibiashara

Hatima ya kisheria ya Bw. Sonko, mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani na mgombea urais aliyetangazwa, imeathiri maisha ya kisiasa ya Senegal tangu maka 2021 na imesababisha matukio kadhaa ya machafuko mabaya. Kulingana na kambi yake, bado ana haki zake za kiraia tangu jaji alipoamuru asajiliwe tena kwenye orodha za wapiga kura katikati ya mwezi Desemba.

Kesi hiyo ilifunguliwa Alhamisi asubuhi bila mshtakiwa lakini mbele ya mawakili wa pande zote mbili, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. Ousmane Sonko, 49, aliyeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019, anashtakiwa na Waziri wa Utalii Mame Mbaye Niang kwa "kuchafua jina lake, matusi na kughushi".

Bw. Sonko alihukumiwa mwezi Machi mara ya kwanza kifungo cha miezi miwili gerezani na kumtaka kulipa faranga za CFA milioni 200 (euro 300,000) kama fidia. Wakati huo, hukumu hiyo ilizua mkanganyiko wa awali wa umma kuhusu athari zake kwa Bw. Sonko kuweza kuwania katika uchaguzi. 

Katika rufaa mwezi wa Mei, na kwa kukosekana kwa Bw. Sonko, mahakama iliimarisha hukumu hiyo, na kuthibitisha fidia ya faranga za CFA milioni 200, lakini ikaongeza hukumu hadi miezi sita.

Hukumu hii inachukuliwa na wengi kama kumzuia asiwezi kuwania kiti cha urais

 kuwania katika uchaguzi wa urais lakini Ibara za 29 na 30 za kanuni za uchaguzi bado zinaonekana kutoa nafasi kwa majadiliano, lakini bado kuna utata kwa kizingiti cha hukumu ya kifungo cha miezi sita. Uamuzi wa Mahakama ya Juu utafunga kesi hii.

Katika utaratibu mwingine, Bw. Sonko alipatikana na hatia mnamo Juni 1 ya uasherati wa mtoto mdogo na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani. Mpinzani hakufika kwenye kesi hiyo na alipatikana na hatia bila kuwepo. Amekuwa gerezani tangu mwisho wa mwezi wa Julai kwa mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na kuitisha uasi na kukemea mambo haya yote kama njama zinazolenga kumuondoa kwenye uchaguzi wa urais.

Utu wa Bw. Sonko unaleta mgawanyiko. Mjadala wake wa kujitawala, wa Kiafrika na wa kijamii, maneno yake dhidi ya wasomi, ufisadi na ushawishi wa kiuchumi na kisiasa unaotekelezwa, kulingana na mwanasiasa huyo, na ukoloni wa zamani wa Ufaransa umemfanya kuungwa mkono sana na vijana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.