Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Senegal: Hatima ya Sonko kuwania kwenye kiti cha urais kujulikana Alhamisi

Mahakama ya Senegal itatoa uamuzi siku ya Alhamisi ikiwa mwanasiasa wa upinzani anayezuiliwa Ousmane Sonko atarejeshwa kwenye orodha ya wapiga kura na ataweza kugombea katika uchaguzi wa urais wa mwezi Februari 2024, jaji ametangaza siku ya Jumanne baada ya kesi hiyo kusikilizwa huko Dakar.

Mahakama ya Juu nchini Senegal ilibatilisha mnamo Novemba 17 hukumu iliyotolewa mwezi Oktoba, ambayo ilimrejesha Bw. Sonko kwenye kinyang'anyiro kwa kubatilisha kuondolewa kwake kwenye orodha ya wapiga kura kufuatia kifungo cha miaka miwili jela mwezi Juni katika kesi ya maadili. Mahakama iliamua kwamba kesi hiyo isikilizwe tena katika mahakaam ya mwanzo.
Mahakama ya Juu nchini Senegal ilibatilisha mnamo Novemba 17 hukumu iliyotolewa mwezi Oktoba, ambayo ilimrejesha Bw. Sonko kwenye kinyang'anyiro kwa kubatilisha kuondolewa kwake kwenye orodha ya wapiga kura kufuatia kifungo cha miaka miwili jela mwezi Juni katika kesi ya maadili. Mahakama iliamua kwamba kesi hiyo isikilizwe tena katika mahakaam ya mwanzo. AFP - MUHAMADOU BITTAYE
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu utaashiria hatua mpya katika mchezo wa kuigiza wa kisheria kati ya kiongozi huyu wa upinzani na Serikali, iliyohusika kwa zaidi ya miaka miwili katika mzozo uliosababishwa na machafuko mabaya. Siku ya Jumanne, mawakili wa pande zote mbili walijadili uamuzi wa kumwondoa Bw Sonko kwenye orodha ya wapiga kura na hivyo kumnyima kumnyima haki ya kugombea kwenye uchaguzi wa urais ambapo atakuwa mmoja wa wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo.

Mahakama ya Juu nchini Senegal ilibatilisha mnamo Novemba 17 hukumu iliyotolewa mwezi Oktoba, ambayo ilimrejesha Bw. Sonko kwenye kinyang'anyiro kwa kubatilisha kuondolewa kwake kwenye orodha ya wapiga kura kufuatia kifungo cha miaka miwili jela mwezi Juni katika kesi ya maadili. Mahakama iliamua kwamba kesi hiyo isikilizwe tena katika mahakaam ya mwanzo.

Bw. Sonko analaani jambo hili na mengine ambayo yeye ndiye mhusika wake kama njama zinazolenga kumtenga katika uchaguzi wa urais. Serikali kwa upande wake inajitetea dhidi ya kuishawishi mahakama.

"Kuna mtu anaitwa Macky Sall (rais wa Senegal) ambaye anataka kwa gharama yoyote kumzuia (Ousmane Sonko) kushiriki katika uchaguzi wa urais," wakili Ousseynou Fall alitangaza katika ufunguzi wa kikao cha wanasheria wa Bw. Sonko. "Wanataka kumzuia kuwa mgombea kwa sababu kama Ousmane Sonko atawania, atashinda katika duru ya kwanza," ameongeza wakili Bamba Cissé, mwanasheria wake mwingine.

Baadaye mchana, mawakili wa serikali waliamua kukataa ombi la Bw. Sonko. Ombi la mpinzani halikubaliki kwa sababu limepitwa na wakati, alisema wakili Adama Fall. "Ousmane Sonko aliwasilisha ombi lake nje ya muda wa siku tano uliowekwa kisheria" ingawa alifahamishwa kuhusu uamuzi wa kufutwa, alisema.

Bw. Sonko aliwekwa gerezani mwishoni mwa mwezi wa Julai kwa mashtaka mengine, ikiwa ni pamoja na kuitisha uasi, njama ya uhalifu kuhusiana na ugaidi na kuhatarisha usalama wa serikali. Hata hivyo Bw. Sonko anapinga tuhuma hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.