Pata taarifa kuu

Mashambulizi katikati mwa Nigeria: Watu 198 waliuawa kulingana na ripoti mpya

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi dhidi ya vijiji katika Jimbo la Plateau, katikati mwa Nigeria, kati ya Jumamosi jioni na Jumanne asubuhi imeongezeka hadi karibu watu 200 waliouawa, mamlaka katika jimbo hilo imesema siku ya Jumatano.

Jimbo la Plateau, Nigeria tayari limekumbwa na mashambulizi mengine mengi. Hapa, wakaazi wanakimbia shambulio la hapo awali mnamo Mei 20, 2023.
Jimbo la Plateau, Nigeria tayari limekumbwa na mashambulizi mengine mengi. Hapa, wakaazi wanakimbia shambulio la hapo awali mnamo Mei 20, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa baraza la serikali ya Bokkos, Monday Kassah, ametangaza kwamba alihesabu "wanakijiji 148 wa Bokkos waliuawa kikatili" wakati wa mkutano wake na makamu wa rais wa Nigeria, ambapo "waliongezwa angalau watu 50 waliuawa" katika vijiji vinne. katika wilaya jirani ya Barkin Ladi, kulingana na Dickson Chollom, mbunge wa eneo hilo, siku ya Jumatano. Ripoti ya awali ilitaja vifo 163.

Kwa sasa kuna "majeruhi 500 na maelfu wamekimbia makazi yao," Monday Kassah aliliambia shirka la habari la AFP siku ya Jumanne. "Si chini ya vijiji 20" kati ya Jumamosi jioni na Jumatatu asubuhi, alisema, akisisitiza kwamba "mashambulizi yaliratibiwa vyema".

Rais wa Nigeria Bola Tinubu aliagiza "vyombo vya usalama kuingilia kati mara moja, kufanua msako kila sehemu ya eneo hilo na kuwakamata wahalifu", baada ya "klaani vikali mashambulizi", ilisema taarifa ya ofisi ya rais siku ya Jumanne.

Wakazi wa mikoa ya kaskazini-magharibi na kati ya Nigeria wanaishi kwa hofu ya mashambulizi ya makundi ya kijihadi na magenge ya wahalifu ambao hupora vijiji na kuua au kuwateka nyara wakaazi.

Kwa miaka mingi, makabiliano makali pia yamekuwa yakiendelea kati ya wafugaji na wakulima katika eneo hili, ambapo wakulima wakiwashutumu wafugaji kwa kupora ardhi yao na mifugo yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.