Pata taarifa kuu

MSF yawahamisha wafanyakazi wake baada ya mapigano kaskazini magharibi mwa Nigeria

Mapigano kati ya makundi yenye silaha na jeshi kaskazini-magharibi mwa Nigeria yamellilazimu shitika la Madaktari Wasi na Mipaka, MSF, kuwahamisha wafanyakazi wake, shitika hilo limesema siku ya Ijumaa.

Magazeti na vituo vya televisheni vya Nigeria vimeripoti mapigano katika kitongoji cha Zurmi baada ya wanamgambo wenye silaha kushambulia makao makuu ya serikali ya eneo hilo na jeshi kujibu. "Baadhi ya wagonjwa wanakataa, kwa hofu, kuondoka hospitalini," amesema Adjide Hermann, naibu mratibu wa MSF huko Zurmi, katika taarifa.
Magazeti na vituo vya televisheni vya Nigeria vimeripoti mapigano katika kitongoji cha Zurmi baada ya wanamgambo wenye silaha kushambulia makao makuu ya serikali ya eneo hilo na jeshi kujibu. "Baadhi ya wagonjwa wanakataa, kwa hofu, kuondoka hospitalini," amesema Adjide Hermann, naibu mratibu wa MSF huko Zurmi, katika taarifa. AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo unaonyesha matatizo yanayokabili mashirika ya kibinadamu kaskazini-magharibi mwa nchi, ambapo wanamgambo wenye silaha, wanaojulikana kama "majambazi", huvamia jamii, huiba vijiji na kutekeleza utekaji nyara ili kulipa fidia.

MSF imesema kuongezeka kwa ghasia katika jimbo la Zamfara kumeifanya kuwahamisha baadhi ya wafanyakazi wake kutoka hospitali ya mji wa Zurmi, ambako mapigano yamekuwa yakiripotiwa kwa siku kadhaa. "Kutokana na hatari kubwa za kiusalama, timu za matibabu za MSF katika zimelazimika kuwahamisha sehemu ya wafanyakazi wao na haziwezi kufanya kazi ipasavyo," taarifa imesema.

Msemaji MSF ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wafanyakazi sita "wasio muhimu" wa kimataifa wamehamishwa, wakati wafanyakazi wengine wa kitaifa na kimataifa walisalia kwenye eneo hilo.

Walipoulizwa na AFP, maafisa wa jimbo la Zamfara na polisi hawakujibu. Lakini gavana wa eneo hilo Dauda Lawal amesema kwenye mtandao wa kijamii wiki hii kwamba "ana wasiwasi mkubwa" kuhusu mashambulizi ya hivi majuzi ya majambazi katika makazi ya Zurmi, Maru na Tsafe huko Zamfara.

Magazeti na vituo vya televisheni vya Nigeria vimeripoti mapigano katika kitongoji cha Zurmi baada ya wanamgambo wenye silaha kushambulia makao makuu ya serikali ya eneo hilo na jeshi kujibu. "Baadhi ya wagonjwa wanakataa, kwa hofu, kuondoka hospitalini," amesema Adjide Hermann, naibu mratibu wa MSF huko Zurmi, katika taarifa.

Ghasia kaskazini-magharibi na kaskazini-kati mwa Nigeria zimesababisha takriban watu milioni moja kuyatorioka makaazi yao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji (IOM).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.