Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Nigeria: Watu 16 wauawa katika shambulio katikati mwa nchi

Watu wenye silaha waliwauwa takriban watu 16 siku ya Jumapili katika shambulio katika kijiji kimoja katikati mwa Nigeria, afisa wa kijeshi amesema. "Kulikuwa namaandamano baada ya tukio hilo, lakini hali imedhibitiwa," Kapteni Oya James ameliambia shirika la habari la AFP. 

Uasi wa wanajihadi ambao umedumu kwa miaka 14 nchini Nigeria ni mojawapo ya changamoto kuu za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Ahmed Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi wa Mei 2023 na ambaye aliahidi kukomesha ghasia hizi kaskazini mashariki.
Uasi wa wanajihadi ambao umedumu kwa miaka 14 nchini Nigeria ni mojawapo ya changamoto kuu za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Ahmed Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi wa Mei 2023 na ambaye aliahidi kukomesha ghasia hizi kaskazini mashariki. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea katika kijiji cha Mushu, katika Jimbo la Plateau, eneo ambalo limekuwa likikumbwa na mivutano ya kidini na kikabila kwa miaka kadhaa.

Watu wenye silaha waliwauwa takriban watu 16 siku ya Jumapili katika shambulio katika kijiji kimoja katikati mwa Nigeria, afisa wa kijeshi alisema. "Kulikuwa na ghasia baada ya tukio lakini hali imedhibitiwa," Kapteni Oya James aliambia AFP.

“Tulikuwa tumelala usiku, ghafla milio mingi ya risasi ilisikika. Tuliogopa kwa sababu hatukutarajia shambulio lolote,” ameeleza Markus Amorudu, mkazi wa kijiji hicho. "Watu walijificha lakini washambuliaji waliteka wengi wetu, wengine waliuawa, wengine walijeruhiwa," ameongeza. Gavana wa jimbo hilo, Caleb Mutfwang, alilaani shambulizi hilo na kulitaja kuwa "la kinyama, la kikatili na lisilo na haki."

Maafisa wa usalama na wanajeshi walitumwa baada ya shambulio hilo kufuatilia eneo hilo na kuzuia fujo. "Hatua madhubuti zitachukuliwa na serikali kupunguza mashambulizi yanayoendelea dhidi ya raia wasio na hatia," amesema Gyang Bere, msemaji wa gavana.

Nchini Nigeria, wakaazi wa mikoa ya kaskazini-magharibi na kati ya nchi hiyo wanaishi katika hofu ya mashambulizi ya makundi ya wanajihadi na makundi ya wahalifu wanaoitwa "majambazi" ambao hupora vijiji na kuua au kuwateka nyara wakaazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.