Pata taarifa kuu

Senegal : Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, ameanza mgomo wa kula

Nairobi – Nchini Senegal, kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, ambaye anaendelea kuzuiliwa gerezani, ametangaza kuanza mgomo wa Kula, baada ya kusitisha mwezi uliopita, wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwakani.

Sonko aliyehukumiwa kifungo mwezi Julai, amemtuhumu rais Macky Sall kwa jaribio la kumzuia asiwanie urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani
Sonko aliyehukumiwa kifungo mwezi Julai, amemtuhumu rais Macky Sall kwa jaribio la kumzuia asiwanie urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani REUTERS - COOPER INVEEN
Matangazo ya kibiashara

Kupitia mitandao yake ya FAcebook na X, Sonko amesema ameanza tena mgomo wa kula ili kuonesha umoja na wanaharakati wengine ambao anasema walikamatwa kinyume cha sheria kwa kutoa maoni yao ya kisiasa.

Mgomo wa kwanza wa kula aliuanza mwishoni mwa mwezi Julai muda tu baada yake kukamatwa, akihusishwa na mashtaka ya kuanzisha uasi, kujihusisha na kundi la kigaidi na kudhoofisha usalama wa kitaifa.

Sonko amekuwa akihusishwa na mashtaka ya kuanzisha uasi, kujihusisha na kundi la kigaidi na kudhoofisha usalama wa kitaifa chini ya uongozi wa rais Macky Sall
Sonko amekuwa akihusishwa na mashtaka ya kuanzisha uasi, kujihusisha na kundi la kigaidi na kudhoofisha usalama wa kitaifa chini ya uongozi wa rais Macky Sall © Montage RFI - AP/Johanna Geron - AFP/John Wessels

Sonko aliyehukumiwa kifungo mwezi Julai, amemtuhumu rais Macky Sall kwa jaribio la kumzuia asiwanie urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, madai ambayo Sall ameendelea kuyakanusha.

Wiki iliyopita, jaji aliamuru Sonko arejeshwe kwenye orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Februari baada ya mamlaka kumwondoa, lakini mawakili wa serikali wakasema watapinga uamuzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.