Pata taarifa kuu

Senegal: Suala la Sonko kugombea kiti cha urais larejeshwa mahakamani

Mahakama mjini Dakar itachunguza kurejeshwa au la kwa mpinzani wa Senegal Ousmane Sonko kwenye orodha za uchaguzi, ambapo kunategemea kugombea kwake kwa uchaguzi wa urais wa mwaka 2024, kulingana na shirika la AFP lililonukuu chanzo cha mahakama siku ya Jumanne.

Ousmane Sonko analani tuhuma hii na zingine zinazomkabili kama njama zinazolenga kumtenga katika uchaguzi wa urais.
Ousmane Sonko analani tuhuma hii na zingine zinazomkabili kama njama zinazolenga kumtenga katika uchaguzi wa urais. Β© AFP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Novemba 17, Mahakama ya Juu zaidi nchini Senegal ilibatilisha uamuzi uliotolewa mwezi Oktoba, ambao ulimrejesha Bw. Sonko kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa kubatilisha uamuzi wa mahakama wa kuondolewa kwake kwenye orodha ya wapiga kura kufuatia kukutwa na hatia katika kesi ya maadili. Mahakama iliamua kwamba kesi hiyo isikilizwe tena kwa mara ya kwanza na mahakama ya Dakar.

Kesi hii imepangwa kusikilizwa tena Desemba 12 saa 8:30 asubuhi (saa za ndani), imebaini taarifa kutoka kwa Mahakama ya Rufaa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP. Bw. Sonko aliondolewa kwenye orodha ya wapiga kura kufuatia kupatikana na hatia mwezi Juni kabla ya kutolewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la utovu wa nidhamu kwa mtoto mdogo.

Bw. Sonko analani tuhuma hii na zingine zinazomkabili kama njama zinazolenga kumtenga katika uchaguzi wa urais.

Kuondolewa kwa Bw. Sonko kunamfanya asiwezi kushiriki uchaguzi wa urais wa 2024 iwapo kutathibitishwa. Hali ambayo ilizua mzozo wa kisheria kati ya mawakili wake na Serikali, iliyohusika kwa zaidi ya miaka miwili katika mzozo na mpinzani ambao ilizua matukio kadhaa ya machafuko mabaya.

Bw. Sonko alifungwa gerezani mwishoni mwa mwezi Julai kwa mashtaka mengine, ikiwa ni pamoja na kuitisha uasi, njama ya uhalifu kuhusiana na ushirikiano na magaidi na kuhatarisha usalama wa taifa. Pia anapinga tuhuma hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.