Pata taarifa kuu

Senegal: Mahakama ya ECOWAS itatoa uamuzi mnamo Novemba 17 kuhusu kuwania kwa Sonko

Mahakama ya Afrika Magharibi imetangaza tarehe 17 Novemba kuwa tarehe ya uamuzi wake wa kurejeshwa kwa mpinzani wa Senegal Ousmane Sonko katika orodha ya wapiga kura, baada ya jina lake kufutwa kwenye orodha ya wagombea urais katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2024.

Jaji wa Ziguinchor (kusini mwa Senegali) alifuta mnamo Oktoba 12, hatua ya serikali ambayo inamzuia Bw. Sonko, aliyechukuwa nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa 2019, kuwa mgombea katika uchaguzi wa Februari 25, 2024.
Jaji wa Ziguinchor (kusini mwa Senegali) alifuta mnamo Oktoba 12, hatua ya serikali ambayo inamzuia Bw. Sonko, aliyechukuwa nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa 2019, kuwa mgombea katika uchaguzi wa Februari 25, 2024. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mawakili wa Bw. Sonko, kiongozi mkuu wa upinzani ambaye yuko katika mzozo uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili na serikali ya Senegal, ambao ulizua matukio kadhaa ya machafuko mabaya, wamepeleka suala hilo kwenye Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ( ECOWAS). Wanaiomba, miongoni mwa mambo mengine, iamuru kurejeshwa kwa Bw Sonko kwenye orodha ya wapiga kura baada ya kuondolewa kwake kufuatia kukutwa na hatia katika kesi ya maadili.

Jaji wa Ziguinchor (kusini mwa Senegali) alifuta mnamo Oktoba 12, hatua hiyo ya serikali ambayo inamzuia Bw. Sonko, aliyechukuwa nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa 2019, kuwa mgombea katika uchaguzi wa Februari 25, 2024.

Wizara ya Mambo ya Ndani kufikia sasa imekataa kumpa Bw Sonko fomu rasmi ambazo zingemruhusu kuchukua ufadhili wake, hatua ya lazima katika kuwasilisha ombi lake la kuwania katika uchaguzi wa urais. Wizara inahoji kuwa uamuzi wa jaji sio wa mwisho na serikali inaweza kukata rufaa. Mahakama ya Juu inatazamiwa kuchunguza rufaa hii mnamo Novemba 17.

Tume ya kitaifa ya uchaguzi, chombo kinachosimamia shughuli za uchaguzi, hata hivyo iliomba Kurugenzi Kuu ya Uchaguzi (DGE), ambayo inategemea Wizara ya Mambo ya Ndani, Oktoba 31 kumrejesha Bw. Sonko kwenye orodha hizo na kuwasilisha faili za ufadhili. Siku hiyo hiyo, DGE ilikataa ombi hilo.

"Ousmane Sonko zimesalia wiki tatu tu (kutoka tarehe ya mwisho iliyowekwa) kuwasilisha fomu za udhamini wake kwa ajili ya kukubaliwa kwa uchaguzi wa urais. Uamuzi wa jaji wa wilaya (ya Ziguinchor) lazima utekelezwe mara moja kwa kuzingatia " dharura", mmoja wa mawakili wa Bw. Sonko, Ciré Clédor Ly, alisema Jumatatu mbele ya Mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.