Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Askari 4 wa vikosi vya usalama wauawa katika shambulizi nchini Nigeria

Askari wanne wa vikosi vya usalama vya Nigeria waliuawa Jumanne katika shambulio la kuvizia la wanajihadi kaskazini mashariki mwa Nigeria, kulingana na sirika la habarila AFPlikinukuu vyanzo kutoka wanamgambo wanaopambana dhidi ya wanajihadi.

Uasi wa wanajihadi ambao umedumu kwa miaka 14 nchini Nigeria ni mojawapo ya changamoto kuu za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Ahmed Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi uliopita wa Mei na ambaye aliahidi kukomesha ghasia hizi kaskazini mashariki.
Uasi wa wanajihadi ambao umedumu kwa miaka 14 nchini Nigeria ni mojawapo ya changamoto kuu za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Ahmed Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi uliopita wa Mei na ambaye aliahidi kukomesha ghasia hizi kaskazini mashariki. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi hao wanaoshirikiana na Islamic State katika Afrika Magharibi (ISWAP), walishambulia timu ya wanajeshi na wanamgambo wanaopinga jihadi waliokuwa wakielekea katika mji wa Monguno, ulioko kilomita 140 kutoka mji mkuu Maiduguri wa Jimbo la Borno, wanamgambo wawili wamesema. 

"Magaidi wa ISWAP walivizia timu ya doria na kuwafyatulia risasi katika kijiji cha Lingir, na kusababisha urushianaji  risasi. Wanajihadi walikuwa wengi na askari wa vikosi vya usalama na washirika wao walilazimika kukimbia," amesema Musa Kaka, kiongozi wa wanamgambo wanaopinga jihadi huko Monguno.  "Wanajeshi wawili na wanamgambo wawili wanaopinga jihadi waliuawa katika mapigano hayo na wengine kadhaa kujeruhiwa," ameongeza.

Uasi wa wanajihadi ambao umedumu kwa miaka 14 nchini Nigeria ni mojawapo ya changamoto kuu za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Ahmed Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi uliopita wa Mei na ambaye aliahidi kukomesha ghasia hizi kaskazini mashariki.

Hata kama ukubwa wa unyanyasaji wa wanajihadi umepungua hatua kwa hatua katika miaka ya hivi karibuni, ISWAP, ambayo ilijitenga na Boko Haram mwaka 2016, bado inasalia katika eneo la Ziwa Chad ambako inakabiliana na kundi lake la zamani mara kwa mara.

ISWAP mara kwa mara hufanya mashambulizi katika maeneo ya vijijini kwenye barabara kuu ya Maiduguri-Monguno, kuwaua na kuwateka nyara madereva wa magari, pamoja na mashambulizi ya mara kwa mara ya Monguno dhidi ya wanajeshi na wanamgambo wanaopinga jihadi.

Katika siku za hivi majuzi, wapiganaji wake wamewaamuru wakaazi wa vijiji vilivyo kando ya barabara kuu kati ya miji ya Gubio, Damasak, Layi, Jamu na Kinsari kuondoka makwao, kulingana na Musa Kaka. Uasi wa wanajihadi nchini Nigeria umesababisha vifo vya watu 40,000 na wengine zaidi ya milioni mbili kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.