Pata taarifa kuu

Nigeria: Vyama vikuu vya wafanyikazi vimeitisha mgomo wa kitaifa

Nairobi – Nchini Nigeira, vyama vikubwa viwili vya wafanyikazi vimewataka wanachama wao kushiriki mgomo na kusalia nyumbani kuanzia leo Jumanne wakati huu mgomo wa kitaifa ukirejelewa.

Vyama hivyo sasa vinatoa wito kwa serikali kuongeza malipo ya kila mwezi kufikia angalau Dolla za Marekani 120 kutoka kwa Dolla 36
Vyama hivyo sasa vinatoa wito kwa serikali kuongeza malipo ya kila mwezi kufikia angalau Dolla za Marekani 120 kutoka kwa Dolla 36 ©
Matangazo ya kibiashara

Mgomo huu unafanyika licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama linalowazuia kufanya hivyo.

Vyama vya Nigeria Labour Congress (NLC) na Trade Union Congress (TUC) vimesema vimechukua hatua hiyo kutokana na kuendelea kupanda kwa gharama ya maisha na kuongezeka kwa bei za mafuta.

Vyama hivyo vimekuwa vikimshinikiza rais Tinubu kurejesha ruzuku kwa bidhaa za petroli, mapango wanaosema ulikuwa unazuia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Serikali mpya rais Bola Tinubu, iliondoa mpango huo kwa misingi kuwa ulikuwa unachukua sehemu kubwa ya fedha za serikali.

Serikali mpya rais Bola Tinubu, iliondoa mpango huo kwa misingi kuwa ulikuwa unachukua sehemu kubwa ya fedha za serikali
Serikali mpya rais Bola Tinubu, iliondoa mpango huo kwa misingi kuwa ulikuwa unachukua sehemu kubwa ya fedha za serikali © Bola Ahmed Tinubu twitter

Mamlaka kwenye taifa hilo ilisema pesa zilizokuwa zinatumika kuweka ruzuku kwa bidhaa za mafuta ziingetumika katika miradi mingine ya serikali.

Vyama hivyo sasa vinatoa wito kwa serikali kuongeza malipo ya kila mwezi kufikia angalau Dolla za Marekani 120 kutoka kwa Dolla 36.

Rais wa chama cha wafanyikazi cha TUC Festus Osifo katika taarifa yake amesisitiza kuwa mgomo huo utaendelea hadi pale ambapo serikali itawajibika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.