Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Nigeria: Wanajihadi waua takriban watu 11 kwenye mashamba ya mpunga kaskazini mashariki

Takriban watu kumi wameuawa na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya mashambulizi ya wanajihadi siku ya Jumapili katika mashamba ya mpunga katika jimbo la Borno (kaskazini mashariki mwa Nigeria), wakaazi wameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

Mashambulizi ya Boko Haram na Islamic State katika Afrika Magharibi dhidi ya wakulima, wakataji miti, wachungaji na hata wavuvi yameongezeka.
Mashambulizi ya Boko Haram na Islamic State katika Afrika Magharibi dhidi ya wakulima, wakataji miti, wachungaji na hata wavuvi yameongezeka. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Wakulima mara nyingi wanalengwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislamu kaskazini-mashariki mwa nchi, ambapo wyamesababisha takriban vifo vya watu 40,000 na zaidi ya milioni mbili kuyahama makazi yao tangu mwaka 2009.

Washambuliaji wanaoshukiwa kuwa wa Boko Haram, walivamia mashamba ya mpunga Jumapili jioni katika wilaya ya Zabarmari, karibu na mji mkuu wa mkoa wa Maiduguri. Kulingana na vyanzo vya ndani vilivyohojiwa na shirika la habari la AFP, waliwachinja wakaazi na kuwateka nyara wengine.

Wakulima katika kijiji cha Karkut wanakuwa kwenye mashamba yao usiku kulinda mazao yao dhidi ya wizi kabla ya kurejea nyumbani asubuhi iliyofuata.

"Tulikuta maiti 11, zote zikiwa zimekatwakatwa na washambuliaji wa Boko Haram," Babakura Kolo, mkuu wa wanamgambo wa eneo hilo wanaopigana na wanamgambo wa Kiislamu walioshiriki katika kuwasafirisha waathiriwa.

Watu kadhaa hawajulikani waliko na waathiriwa wanne walinusurika kifo na kupelekwa hospitalini.

Sala na ibada ya mazishi ya wahanga 11 yamefanyika katika Msikiti Mkuu wa Zabarmari Jumatatu alasiri. Makamu wa gavana alishiriki trukio hilo, kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani.

Mashambulizi ya Boko Haram na Islamic State katika Afrika Magharibi (Iswap) dhidi ya wakulima, wakataji miti, wachungaji na wavuvi yameongezeka, huku wanamgambo wa Kiislamu wakiwashutumu kwa kusambaza taarifa kwa jeshi na wanamgambo wa ndani wanaopambana nao.

Mnamo Desemba 2020, Boko Haram iliwaua wakulima 76 huko Zabarmari, mauaji mabaya zaidi ya wakulima kulingana na mamlaka ya ndani.

Wapiganaji wa kijihadi wameshindwa vita kaskazini mashariki mwa Nigeria lakini wanaendelea kushambulia jamii za vijijini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.