Pata taarifa kuu

Nigeria: Karibia watu 25 wamefariki katika ajali ya barabarani

Watu 25 wamefariki nchini Nigeria katika jimbo la Niger baada ya gari walimokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kuanguka.

Ajali hiyo ilihusisha lori ambalo lilikuwa likielekea katika mji wa kibiashara wa Lagos likitoka katika jimbo la Sokoto
Ajali hiyo ilihusisha lori ambalo lilikuwa likielekea katika mji wa kibiashara wa Lagos likitoka katika jimbo la Sokoto AFP
Matangazo ya kibiashara

Lori hilo ambalo lilikuwa likielekea katika mji wa kibiashara wa Lagos likitoka katika jimbo la Sokoto , lilikuwa likiendeshwa kwa kasi likiwa na abiria kupita kiasi na mizigo, kwa mujibu wa shirika la kushugulikia usalama wa barabarani nchini humo.

Abiria wengine wanauuguza majeraha mbaya baada ya kunusurika kutoka kwenye ajali hiyo.

Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumanne usiku japokuwa imethibitishwa na mamlaka siku ya Jumatano.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amezitaka mamlaka husika kuhakikisha waliojeruhiwa wanapata matibabu yanayohitajika.

Gavana wa jimbo la Niger Mohammed Bago ametoa agizo la kupiga marafuku malori kuwasafirisha abiria.

Ajali nyingi za barabarani hushudiwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika haswa wakati wa msimu wa mvua na kuelekea sikukuu za krisimasi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.