Pata taarifa kuu

Walinda amani: Umoja wa Mataifa na AU zazingatia mustakabali wa misheni za kulinda amani

Mustakabali wa operesheni za ulinzi wa amani barani Afrika unazidi kuwa mashakani wakati Mali ilipoomba kuondoka kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa (MNINUSMA) mnamo mwezi Juni 2023 na DRC inaomba kwa moyo dhati MONUSCO kuanza kuondoka nchini humo kunzia mwezi huu wa Desemba.

Kambi ya Monusco katika kata ya Boikene mjini Béni  Novemba 16 2018. (picha ya maonyesho)
Kambi ya Monusco katika kata ya Boikene mjini Béni Novemba 16 2018. (picha ya maonyesho) EUTERS/Samuel Mambo
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Umoja wa Mataifa unashangaa jinsi ya kukabiliana na vitisho kutoka kwa magaidi na makundi yenye silaha katika bara la Afrika. Na jinsi ya kuchukua nafasi ya walinzi wa amani. Hili lilikuwa swali katika kiini cha mkutano wa saba wa uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (AU). Taasisi hizo mbili pia zimetia saini makubaliano ya kuheshimu haki za binadamu.

Kwa upande wa viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, wanasema misheni za kulinda amani kama zilivyofikiriwa miongo kadhaa iliyopita hazina umuhimu tena wa kukabiliana na ghasia zinazoongezeka. Ni wakati wa kubadili mtindo, anasema Moussa Faki, mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika: “Asili ya tishio hili katika bara la Afrika inahitaji jibu linalofaa. Sio kwa kukosa kuwa na pendekezo sisi, Waafrika, kuweka tayari vikosi. "

AU yenye uwezo

Lakini, amesema tena, “misheni hizi za Afŕika lazima zifadhiliwe na ŕasilimali za Umoja wa Mataifa. Hili ni tishio kwa amani na usalama, na hili ni jukumu la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.” Swali la ufadhili linawarudisha nyuma wanachama watano wa kudumu huko New York ambao hawaangalii kwa jicho zuri uondoaji wa walinda amani "unaotarajiwa". Hata hivyo, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anatuhakikishia: Umoja wa Afrika una uwezo wa kutekeleza misheni hizi.

"Matumaini"

"Sheria za kufuata ambazo Umoja wa Afrika umeweka zinaendana kikamilifu na zetu," anasisitiza. Na makubaliano tuliyofikia leo kuhusu haki za binadamu ni hakikisho zaidi kwamba tunaweza kuamini Umoja wa Afrika kuandaa operesheni za kulinda amani barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.