Pata taarifa kuu

Abiy Ahmed: Ethiopia 'haitadai maslahi yake kupitia vita' katika Bahari Nyekundu

Ethiopia haina nia ya kuivamia nchi nyingine na "kamwe haitatetea maslahi yake kupitia vita", amesema Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed siku ya Alhamisi, siku chache baada ya hotuba ambayo ilizua wasiwasi juu ya uwezekano wa madai ya Addis Ababa kwa Bahari Nyekundu.

Hatua ya Abiy Ahmed kuanzisha tena uhusiano na Eritrea ulimfanya atunukiwe Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo mwaka 2019, lakini umaarufu wake ulianguka alipotuma jeshi la shirikisho kuwaondoa mamlakani viongozi wa mkoa wa kaskazini wa Tigray ambao waliingia katika uasi.
Hatua ya Abiy Ahmed kuanzisha tena uhusiano na Eritrea ulimfanya atunukiwe Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo mwaka 2019, lakini umaarufu wake ulianguka alipotuma jeshi la shirikisho kuwaondoa mamlakani viongozi wa mkoa wa kaskazini wa Tigray ambao waliingia katika uasi. AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Oktoba 13, Bw. Abiy alibaini katika hotuba ya televisheni kwamba "kuwepo kwa Ethiopia kama taifa kunahusishwa na Bahari Nyekundu", kwamba nchi yake inahitaji bandari na kwamba "amani" katika eneo hilo inategemea "kugawana uwiano" kati ya nchi Ethiopia na majirani zake.

Ethiopia, nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika ikiwa na takriban wakaazi milioni 120, haina ufikiaji wa moja kwa moja kwenye Bahari Nyekundu, moja ya njia kuu za biashara ya ulimwengu, tofauti na majirani zake Eritrea na Djibouti.

Hata kama alithibitisha "kutotaka kuingilia masuala" ya nchi nyingine na kutaka "kwa amani" kusisitiza ombi lake la bandari kwenye Bahari Nyekundu, hotuba ya Bw. Abiy iliwatia wasiwasi baadhi ya waangalizi, hasa katika muktadha wa mivutano inayoonekana na nchi jirani ya Eritrea.

"Ethiopia haijawahi kuivamia nchi yoyote na haitafanya hivyo katika siku zijazo," amehakikisha Bw. Abiy katika hotuba aliyoitoa leo Alhamisi katikati mwa Addis Ababa, katika hafla ya "Siku ya Majeshi ya Ulinzi" inayoadhimishwa kila mwaka. "Mahitaji yetu ya hivi majuzi ya kuingia baharini yamezua hofu kwamba Ethiopia itaongoza uvamizi. Nataka kuhakikisha kwamba Ethiopia haitatetea maslahi yake kupitia vita," ameo,geza Waziri Mkuu wa Ethiopia.

 Hatua ya Abiy Ahmed kuanzisha tena uhusiano na Eritrea ulimfanya atunukiwe Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo mwaka 2019, lakini umaarufu wake ulianguka alipotuma jeshi la shirikisho kuwaondoa mamlakani viongozi wa mkoa wa kaskazini wa Tigray ambao waliingia katika uasi. Vita huko Tigray, vilivyodumu kutoka mwezi Novemba 2020 hadi Novemba 2022, vilisababisha vifo vya mamia ya watu.

Ethiopia ya kisasa ilipata ufikaji wa Bahari Nyekundu kwa muda mfupi, ilipoichukua hatua kwa hatua Eritrea, koloni la zamani la Italia, katika miaka ya 1950. Imepoteza ufikiaji huu tangu mzozo kati ya nchi hizo mbili kati ya mwaka 1998 na 2000, miaka kadhaa baada ya Eritrea kuwa huru mnamo mwaka 1993 na Ethiopia sasa inategemea bandari ya Djibouti kwa mauzo na uagizaji wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.