Pata taarifa kuu

Brics: Mataifa ya Ethiopia na Iran yapongeza hatua ya kupewa uanachama

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy amefisia tangazo la uongozi wa Brics kuwa nchi yake itakuwa mwanachama wa muungano huo, hatua ambayo pia imepongezwa na nchi ya Iran.

Vladimir Putin wa Urusi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Vladimir Putin wa Urusi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa X zamani ukijuliakana kama twitter, Abiy Ahamed amesema nchi yake iko tayari kushirkiana na mataifa mengine ya muungano huo katika ulingo wa kimataifa.

Kiongozi huyo aidha amesema hatua hii ni muhimu kwa raia wa nchi yake na kuwapongeza baada ya tangazo la Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano wa kilele wa BRICS kuwa nchi yao ni miongoni mwa nchi sita mpya zitazopata uanchama wa muungano huo.

Ethiopia, nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, itakuwa mwanachama kamili kuanzia Januari 1, 2024, pamoja na Argentina, Misri, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Brics imetoa nafasi kwa wanachama wapya sita kujiunga na muungano huo mwaka ujao
Brics imetoa nafasi kwa wanachama wapya sita kujiunga na muungano huo mwaka ujao REUTERS - ALET PRETORIUS

Katika upande mwengine, mshauri mkuu wa rais wa Iran naye pia amepongeza hatua ya nchi yake kujumuishwa katika muungano huo wa mataifa ya Brics.

Tangazo hilo la Alhamis limekuja wakati huu Iran ikiwa mbioni kutafuta washirika wapya kujaribu kumaliza upweke wake katika nyanja ya kimataifa.

Kwa mujibu wa rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, mataifa mapya yatajiunga rasimi mwezi Januari mwaka ujao
Kwa mujibu wa rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, mataifa mapya yatajiunga rasimi mwezi Januari mwaka ujao REUTERS - ALET PRETORIUS

Idadi kubwa ya mataifa yalikuwa yametuma maombi rasmi ya kujiunga na Brics, ambayo inawakilisha robo ya uchumi wa dunia na zaidi ya watu bilioni tatu.

Baadhi ya wakuu wengine 50 wa nchi na serikali wanahudhuria mkutano huo mjini Johannesburg, ambao unakamilika siku ya Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.