Pata taarifa kuu

Ethiopia: Jeshi la serikali limewarejesha nyuma wapiganaji wa Amhara

Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wamedaiwa kuwarudisha nyuma wapiganaji waasi katika eneo linalokabiliwa na machafuko la Amhara.

Mamlaka katika eneo hilo imeanza kuripoti  kurejeshwa kwa utulivu
Mamlaka katika eneo hilo imeanza kuripoti kurejeshwa kwa utulivu AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi katika eneo hilo wamethibitisha hatua hiyo inayokuja wakati huu mamlaka katika eneo hilo ikiripoti kuaanza kurejeshwa kwa utulivu.

Shirika la ndege la Ethiopia  nalo pia limetangaza kurejelewa kwa shughuli zake za usafiri kaskazini mwa taifa hilo haswa katika mji mkuu wa Amhara Bahir Dar na  Gondar kuaanzia leo Alhamis baada ya kusitishwa siku ya Jumanne ya wiki hii.

Serikali ya waziri mkuu wa taifa hilo Abiy Ahmed, wiki iliyopita ilitangaza muda wa dharura wa kipindi cha miezi sita katika jimbo la Amhara baada ya kutokea kwa mapigano mbaya kati ya wapiganaji wa eneo hilo na jeshi la seriklai ya shirikisho.

Machafuko haya mapya nchini humo yanakuja ikiwa imepita miezi tisa tangu kumalizika kwa mapigano mengine yaliodumu kwa kipindi cha miaka miwili katika jimbo jirani la Tigray.

Wasiwasi imekuwa ikiongezeka tangu mwezi Aprili baada ya serikali ya shirikisho kutangaza kuvunjwa kwa vikosi vya majimbo nchini humo.

Hatua hiyo ya serikali ilisababisha maandamano katika eneo la Amhara, raia wake wakisema hatua hiyo ingedhoofisha eneo lao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.