Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Misri: Watalii wawili wa Israel na Mmisri mmoja wauawa na afisa wa polisi

Watalii wawili wa Israel na Mmisri mmoja wameuawa siku ya Jumapili na afisa wa polisi huko Alexandria, kwenye pwani ya kaskazini ya Misri, vimesema vyombo vya habari vya ndani vilivyo karibu na vyombo vya usalama, katikati ya vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina.

Watalii (Mume na mkewe) wakipiga picha huko Alexandria, mwaka wa 2019.
Watalii (Mume na mkewe) wakipiga picha huko Alexandria, mwaka wa 2019. © Maya Alleruzzo / AP
Matangazo ya kibiashara

"Afisa wa polisi huko Alexandria ametumia silaha yake ya kibinafsi na kufyatua risasi kiholela dhidi ya kundi la watalii wa Israeli (...). Watalii wawili wameuawa, pamoja na Mmisri mmoja na afisa wa polisi amekamatwa," televisheni ya Extra News imesema, ikitoa "chanzo cha usalama."

Misri, nchi jirani ya Israeli na nchi muhimu mpatanishi katika kila mlipuko mpya wa ghasia kati ya Israel na Gaza, ambayo pia inapakana na Israel na Gaza, Palestina, ni taifa la kwanza la Kiarabu kurekebisha uhusiano wake na Israel, mwaka 1979. Ikiwa nchi hizi mbili zimezingatia amani, kwa mfadhaiko mkubwa wa mataifa mengine ya Kiarabu, katikamitaa ya Misri, Israeli bado ni adui mkubwa.

Mnamo Juni, wanajeshi watatu wa Israeli waliuawa na "polisi wa Misri" ambaye "alijipenyeza" kutoka Misri na kuingia Israeli kabla ya kupigwa risasi na kufa, kulingana na msemaji wa jeshi la Israeli. Kulingana na toleo la Misri, afisa wa "vikosi vya usalama akifukuzana na walanguzi wa dawa za kulevya" alivuka kizuizi cha mpaka. Kulifuata "urushianaji wa risasi kitendo ambacho kimligharimu maisha ya watu watatu upande wa Israeli" pamoja na Mmisri mmoja.

Watalii wengi wa Israeli hutembelea nchini Misri

Baada ya tukio hilo, rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mamlaka za nchi hizo mbili zimethibitisha kwa mara nyingine tena ushirikiano wao. Kwa kurejeshwa kwa uhusiano wa nchi hizi mbili, Cairo iliweza kuchukuwa eneo la Sinai, lililokaliwa na Israeli tangu kushindwa kwa Waarabu mnamo 1967.

Makubaliano ya amani yalifuatia vita vya Oktoba 1973, vilivyochukuliwa kuwa "ushindi" mkubwa nchini Misri. Hamas ilianzisha mashambulizi yake ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya Israel siku ya Jumamosi, miaka hamsini baada ya vita vya 1973.

Watalii wengi wa Israeli hutembelea Misri, hasa katika eneo la Sinai, ambapo wanaweza kuingia kwa gari. Katika miaka ya hivi karibuni, Israel na Misri zilizindua safari za anga za moja kwa moja kati ya Tel Aviv na Sharm el-Sheikh, eneo la mapumziko la bahari kwenye Bahari Nyekundu, wakati safari za ndege za moja kwa moja tayari zinaunganisha Tel Aviv hadi Cairo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.