Pata taarifa kuu

Marekani yasisitiza kuunga mkono Israel, Misri yaanza mfululizo wa mawasiliano ya kikanda

Ulimwengu unatazama mapigano yaliyozuka Jumamosi hii, Oktoba 7, kati ya Hamas na Israel, na mashambulizi ya wapiganaji wa Palestina mwanzoni mwa siku na wanajeshi wa Israel kulipiza kisasi katika Ukanda wa Gaza. Marekani kwa haraka imetangaza kuunga mkono mshirika wake Israel, huku Misri na Uturuki zikijiona kuwa wapatanishi zaidi katika mgogoro huo.

Rais wa Marekani Joe Biden alisisitiza uungaji wake mkono kwa Israeli kutoka Ikulu ya Marekani mnamo Oktoba 7, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden alisisitiza uungaji wake mkono kwa Israeli kutoka Ikulu ya Marekani mnamo Oktoba 7, 2023. AP - Manuel Balce Ceneta
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za hivi punde zinabaini zaidi ya vifo 200 kwa upande wa Israel na vifo visivyopungua 232 kwa upande wa Wapalestina, wakati mapigano yalikuwa bado yakiendelea jioni ya Oktoba 7. Kutokana na kuzuka kwa ghasia kati ya Hamas na Israel, jumuiya ya kimataifa imeelezea kusikitishwa na mapigano hayo mapya. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga mkutano wa dharura siku ya Jumapili. Na siku nzima ya Jumamosi, huku makombora yakianguka pande zote mbili.

Washington, "msaada usiotetereka" kwa Israeli

Mshirika wa muda mrefu wa Israeli, Washington imekumbusha kwamba msaada wake "uko tayari". Katika taarifa, Joe Biden amesema kuwa "Marekani inasimama kidete na Israel," anaeleza Loubna Anaki mwandishi wetu mjini New York. Rais wa Marekani ameshutumu mashambulizi yaliyofanywa na Hamas na kuandika, katika taarifa, kwamba "ugaidi haukubaliki". Baadaye, katika hotuba fupi kutoka Ikulu ya White House, mkuu wa nchi wa Marekani alihakikisha kwa maneno kwamba wako tayari kwa "msaada usiotetereka" kwa Israeli.

Joe Biden pia alizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye ameahidi "msaada wote muhimu". Msaada uliothibitishwa mapema kidogo na msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa; Adrienne Watson ambaye alisema Washington inalaani bila shaka mashambulizi yanayolenga raia wa Israel.

Maafisa wa Marekani wanasema wanawasiliana mara kwa mara na wenzao wa Israel. Waziri wa Ulinzi wa Marekani aliandika kuwa, katika siku zijazo, Pentagon itahakikisha kwamba Israel inapata inachohitaji ili kujilinda. Kama ukumbusho, Marekani ndiyo mtoaji mkuu wa misaada ya kijeshi kwa Israel.

Misri imezidisha mazungumzo ili kupunguza mzozo mpya

Ndani ya Umoja wa Ulaya, uvamizi wa Hamas unalaaniwa vikali. Ursula von der Leyen, rais wa Tume ya Ulaya, alilaani mashambulizi yanayofikia kwenye kiwango cha "ugaidi". Josep Borrell, mkuu wa diplomasia ya Ulaya, alishutumu utekaji nyara "wa kutisha" wa raia wa Israeli na kuweka upya "mshikamano" wa Umoja wa Ulaya na Israeli. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron "amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi" ya Hamas.

Misri, kama mpatanishi wa jadi kati ya Palestina na Israeli, imeanzisha safu ya mazungumzo ya kikanda na kimataifa ili kutafuta kudhibiti mzozo wa sasa, anaelezea Alexandre Buccianti mwandishi wetu kutoka Cairo. Juhudi za Misri zinalenga, awali, kukomesha kuongezeka kwa ghasia na hatari kwa raia. Waziri wa mambo ya nje wa Misri aliwasiliana na makamu wa rais wa Kamisheni ya Ulaya, pamoja na viongozi wenzake wa Ghuba ya Kiarabu.

Mazungumzo mengine yamepangwa na Marekani, mfuasi mkuu wa Israeli, ili kushawishi taifa la Kiyahudi kuweza kujizuia. Wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya wakuu wa diplomasia ya Misri na Marekani Sameh Choukri na Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisisitiza "udharura wa kufikiwa kusitishwa mara moja kwa mashambulizi ya kutisha ya magaidi wa Hamas dhidi ya Israel, alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller.

Misri, hata hivyo na kwa sababu hizo hizo, imewasiliana na wafadhili wa kifedha wa Hamas kama vile Qatar. Mazungumzo ya moja kwa moja na Iran, ambayo inasaidia Hamas kwa silaha - na ambayo ilikaribisha operesheni ya "Mafuriko ya Al-Aqsa" - yamesitishwa kwa sasa, hata kama uhusiano kidogo umeanza kati ya Cairo na Tehran. Hatimaye, inakadiriwa, katika mji mkuu wa Misri, kwamba kuwepo kwa wafungwa wa Israel huko Gaza ni ni suala jipya ambalo litapaswa kuzingatiwa katika upatanishi.

Saudi Arabia inataka "mchakato wa amani wa kuaminika"

Nchini Saudi Arabia, Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa wito wa "kukomeshwa mara moja kwa ghasia kati ya makundi ya Wapalestina na vikosi vya Israel vinavyokalia kwa mabavu" baadhi ya maeneo ya Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.