Pata taarifa kuu

Misri: Waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Sisi kuwania tena wakamatwa

Nairobi – Karibia raia 400 nchini Misri wamekamatwa kwa kuhusishwa na maandamano yaliyotokea baada ya rais Abdel Fattah al-Sisi, kutangaza kuwania urais kwa awamu ya tatu, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Uchaguzi wa urais nchini Misri umeratibiwa kufanyika mwezi Desemba
Uchaguzi wa urais nchini Misri umeratibiwa kufanyika mwezi Desemba AFP - KHALED DESOUKI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya rais Sisi, siku ya Jumanne ilionekana kuzua ghadhabu kutoka kwa raia kwenye taifa hilo, baadhi ya vídeo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikonyesha maandamano yaliofanyika katika mji wa Marsa Matrouh, kaskazini mashariki mwa taifa hilo.

Baadhi ya waandamanaji katika vídeo hiyo wanasikika wakiimba nyimbo za kumtaka rais Sisi kuondoka pamoja na utawala wake.

Video nyengine zilionyesha makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.

Kiongozi huyo wa zamani wa jeshi amekuwa madarakani tangu kuangushwa kwa utawala wa Mohammed Morsi, mwaka wa 2013 kufuatia maandamano makubwa dhidi ya uongozi wake.

Wanaharakati kwenye taifa hilo wanasema awamu ya pili ya uongozi wake rais Sisi imekabiliwa na visa vya ukandamizaji wa upinzani na kushuka kwa uchumi wa taifa hilo.

Uchaguzi wa urais nchini Misri umeratibiwa kufanyika mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.