Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Wanafunzi watano watekwa nyara Nigeria

Wanafunzi watano wa kike walitekwa nyara na watu wenye silaha kaskazini mwa Nigeria siku ya Jumatano, siku kumi baada ya watu wengine ishirini kutekwa nyara katika eneo jirani, polisi imesema.

Mwishoni mwa mwaka wa 2020 na mwanzoni mwa mwaka wa 2021, makundi yenye silaha yalilenga hasa shule, shule za mabweni na vyuo vikuu vilivyoko vijijini.
Mwishoni mwa mwaka wa 2020 na mwanzoni mwa mwaka wa 2021, makundi yenye silaha yalilenga hasa shule, shule za mabweni na vyuo vikuu vilivyoko vijijini. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Karibu saa mbili asubuhi, watu wanaoshukiwa kuwa magaidi waliwateka nyara wanafunzi watano kutoka Chuo Kikuu cha Shirikisho," msemaji wa polisi wa jimbo la Katsina Aliyu Abubakar Sadiq alisema katika taarifa Jumatano jioni. Operesheni ya polisi kuwatafuta mateka hao inaendelea, alisema na kuongeza kuwa mtu mmoja anayehusika na utekaji nyara huu amekamatwa.

Utekaji nyara huu unakuja chini ya wiki mbili baada ya watu thelathini kutekwa nyara katika jimbo jirani la Zamfara, wakiwemo angalau wanafunzi 24 wa kike karibu na chuo kikuu kingine. Vikosi vya usalama hadi sasa vimefanikiwa kuwaokoa mateka kumi na sita wakiwemo wanafunzi kumi na watatu.

Majimbo mengi ya kaskazini, ikiwa ni pamoja na Zamfara na Katsina, yamekumbwa na ghasia kutoka kwa majambazi wanaofanya mashambulizi kwenye vijiji, kuua na kuwateka nyara wakazi na kuchoma moto nyumba baada ya kuwapora.

Mwishoni mwa 2020 na mwanzoni mwa 2021, magenge haya yalilenga hasa shule, shule za mabweni na vyuo vikuu vilivyoko katika maeneo haya ya vijijini na kutekeleza utekaji nyara mkubwa ili kupata fidia. Utekaji nyara huu kwa kiasi kikubwa umechangia kwa wanafunzi wanaoacha shule, hasa miongoni mwa wasichana, katika mikoa hii maskini sana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.